WALIMU WA SEKONDARI KUFUNDISHA S/MSINGI SI KUSHUSHA CHEO
Taarifa
ya mkuu wa kitengo cha mawasiliano Ofisi ya Rais (Utumishi), Florence
Lawrence imesema Serikali kuwapangia baadhi ya walimu wa sekondari
kufundisha shule za msingi ni moja ya hatua za kuongeza ufanisi na
kuleta mgawanyo sawa wa walimu katika shule hizo.
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk Laurean
Ndumbaro amekaririwa katika taarifa hiyo iliyotolewa jana Februari
20,2018 akisema hatua hiyo haimaanishi kuwa walimu wanaotoka katika
shule ya sekondari kwenda kufundisha msingi wameshushwa cheo.
Dk Ndumbaro ametoa ufafanuzi huo katika kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako.
Amesema lengo la Serikali ni kuondoa upungufu wa walimu katika shule za msingi na kuimarisha utoaji wa elimu.
Katibu
mkuu ameainisha kuwa sifa za kufundisha na kiwango cha elimu zinaendana
na mabadiliko yanayotokea duniani, hivyo mwalimu mwenye elimu ya
kiwango cha Shahada ya kwanza kufundisha shule ya msingi isionekane ni
jambo la ajabu.
Dk
Ndumbaro amewaambia watumishi wa umma kuwa, maendeleo katika sekta
yoyote, ikiwamo ya elimu yanakuja na mabadiliko hivyo wayapokee na
kufanya kazi ili kufikia lengo.
Post a Comment