WAISHIO NA VIRUSI VYA UKIMWI WAIOMBA SERIKALI KUWASAIDIA
BARAZA la Taifa la watu wanaoishi na virusi
vya Ukimwi (Nacopha) wameiomba Serikali kuzielekeza halmashauri zote
nchini kuhakikisha zinatenga fedha kwa ajili kulisaidia kundi hilo ili
liweze kuachana na utegemezi katika jamii.
Wametoa Ombi hilo hivi karibuni wakati
walipotembelewa na kamati ya Bunge inayoshughulikia Masuala ya Ukimwi na Madawa
ya Kulevya ambayo ilifanya ziara wilayani hapa.
Afisa Mtendaji wa Baraza hilo Deogratius
Rutatwa alisema kundi la watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi linapaswa
kutengewa fedha kwa ajili ya kujiendesha kama yalivyo makundi mengine.
Alisema fedha hizo zitawasaidia kuanzisha na
kuendeleza miradi ya kijasirismali katika konga zao kwa lengo la kuwainua
kiuchumi na kuondokona na utegemezi kwenye familia na jamii kwa ujumla.
Rutatwa alisema watu wanaoishi na Virusi
vya Ukimwi wana uwezo wa kufanya shughuli za uzalishaji mali kama walivyo
watu wengine ikiwa watapatiwa mtaji na nyenzo za kijasiriamali.
“Kupitia ziara hii mnaweza kujionea ni
kwa jinsi gani 'Waviu' (watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi) ambao waliwezeshwa
na NMSF kwa mwaka wa fedha 2014/15 wameweza kuendeleza mitaji hiyo na kubadili
maisha yao"alisema
Hata hivyo aliwataka watu wanaoishi na Virusi
vya Ukimwi kushiriki katika kutoa huduma kwa waviu ndani ya jamii na
kuendelea kuihamasisha jamii kuepukana na Ugonjwa huo.
Alisema baraza hilo kupitia unaofadhiliwa na USAID
Sauti yetu litaendelea kuwahamasisha waviu nchini kujiunga katika vikundi ili
kuunganisha nguvu waweze kujikwamua kiuchumi.
Akisoma risala kwa niaba ya wenzake katibu wa
wa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, Konga ya Mbozi Joyce Chamba alisema
Changamoto kubwa inayolikumba kundi hilo ni kipato duni.
Alisema wengi wao wanatoka kwenye kaya
masikini hivyo wanahitaji Msaada kutoka serikalini na kwa wadau wengine ili
waweze kujikwamua kiuchumi.
"Tukitengewa bajeti tutafikia lengo la
sifuri tatu ambalo ni kuhakikisha vifo vitokanavyo na Ukimwi vinafikia asilimia
sifuri, pamoja nakutokomeza maambukizi Mapya na kutokomeza Unyanyapaa
hadi kufikia siuri ifikapo mwaka 2030,"
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya
Bunge inayoshughulikia Ukimwi na Madawa ya Kulevya Dr. Jasmini Bunga alipongeza
kazi nzuri ya Baraza na wadau wengine na kuwataka kuendelea kuihamasisha jamii
kwenye mapambano ya Ukimwi.
Hata hivyo alishauri kuwepo kwa sheria ya
kuwalazimisha watu kupima Ukimwi kwani itasaidia mkakati wa Serikali kudhibiti
ugonjwa huo.
Alisema hatua hiyo itasaidia serikali kupa
takwimu sahihi za watu waishio na virusi vya Ukimwi nchini itaandaa utaratibu
mzuri wa kutoa huduma bora kwao.
Post a Comment