WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI ZA MKOA WA MBEYA KIKAANGONI
MBEYA
WAKUU wa
Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za mkoani Mbeya sasa wako kikaangoni baada
ya kutakiwa wajieleze ni kwa nini wameshindwa kutekeleza agizo la Kupiga Chapa
Mifugo.
Wakuu wa
wilaya na Wakurugenzi watatakiwa kuwasilisha barua za kujieleza leo(Januari 30)
kwa Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mbeya kisha na yeye aambatanishe na takwimu za
utekelezaji kwa kila Halmashauri na kuzituma kwa waziri mwenye dhamana.
Mkuu wa
mkoa wa Mbeya,Amos Makalla alitoa agizo hilo jana(Januari 30) alipokuwa kwenye
Kikao cha Kuandikishana mikataba kati ya Shirika la Ujerumani la Giz na
Hospitali na vituo vya Afya vilivyoingia Ubia wa utoaji huduma za Afya na
Serikali ambapo pia wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri pia
walihudhuria.
Makalla
alisema kati ya Halmashauri zote za mkoani hapa ni moja tu ya Jiji la Mbeya
iliyotekeleza agizo hilo kwa asilimia 100 huku nyingine zote zikiwa zimesuasua.
mkuu wa mkoa wa mbeya Amos Makalla |
Alisema
Halmashauri ya wilaya ya Mbarali imetekeleza kwa asilimia 85,Kyela asilimia 84,Mbeya
vijijini asilimia 81,Busokelo asilimia 73,Chunya asilimia 42 na Rungwe ni ya
mwisho ambapo imetekeleza kwa asilimia 27 pekee.
“Mpaka
kesho saa nane mchana niwe nimepokea baru na siyo za wilaya ni mtu mmoja mmoja
aandike.Yaani mkuu wa wilaya anaandika yak wake na mkurugenzi yak wake ujieleze
ni kwa nini haujatekeleza.Wala kusiwe kusingiziana .Mlete niambatanishe na
takwimu zilizopo kisha ntawasilisha keshokutwa kwa waziri mwenye dhamana”
“Wakati
tunaanza kuna Halmashauri zilitafsiri kuwa ni agizo la mkuu wa mkoa.Sisi
tulikuwa watu wa mwanzoni kabisa,tulizindua mara tu baada ya mkoa wa Morogoro
kuzindua.Na kila wakati nimekuwa nikiwakumbusha lakini wapi.Sasa mjieleze
wenyewe!”alisisitiza
Post a Comment