CHADEMA YAPATA PIGO KYELA
KYELA
SIKU Chache
baada ya waziri mkuu mtaafu na mjumbe wa kamati kuu Chadema Edward Lowasa
kumpongeza Rais John Magufuli,kwa utendaji kazi mzuru,hatimaye wanachama 52
akiwemo mwenyekiti wa kitongoji na mke wa mwenyekiti wa kijiji kupitia
Chadema,wamehamia chama cha mapinduzi (CCM).
Lowasa
ambaye alikuwa mgombea urais kupitia Ukawa, siku za hivi karibuni alienda Ikulu
kumtembelea Rais Magufuli kuzungumza mambo mbalimbali ambapo alizungumza
wazi akisifu kazi nzuri inayofanywa na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa
na Rasi Magufuli na kuzua minong’ono huku baadhi watu kuoji sababu ya kusifu.
Akizungumza hapo juzi siku ya jumapili katika hafla ya kumpokea aliyekuwa mwenyekiti wa kitongoji cha Lugoje
kijiji cha Tenende kata ya Mwaya Adamson Mwangomo (CHADEMA) katibu wa siasa
itikadi na uenezi ccm wilaya,Emmanuel Mwamulinge,alisema mwenyekiti
huyo,ameamua kurudi ccm kwa ridhaa yake mwenyewe.
Alisema
mbali na mwenyekiti huyo pia uongozi wa ccm kata ya Ndobo imewapokea wanachama
50 kutoka Chadema akiwemo mke wa mwenyekiti wa kijiji cha Bwato,kupitia
Chadema,ambapo CCM wilaya imepanga kuwatamburisha na kuwapa kadi siku ya
sherehe za maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa chama.
Akizungumzia
sababu ya kuhama kwake Adamson Mwangomo,alisema bila kupepesa macho na
kushawishiwa na mtu,ameamua kuiacha nafasi hiyo ya uenyekiti na kuhamia Ccm kwa
kuwa ameridhika na utawara wa serikali ya awamu ya tano na pia umakini wa
viongozi wa ccm wilaya.
Katibu wa ccm
wilaya,Christina Kibiki,alisema licha ya mwenyekiti huyo kuhamia ccm,pamoja na
wanachama wengine 50 akiwemo mke wa mwenyekiti kupitia Chadema,alisema wapo
wengine wengi wamejiunga na ccm ambapo siku ya maadhimisho ya kuzaliwa chama
watawapatia kadina utaratibu mungine.
Mwenyekiti
wa Chadema wilayani humo,Lumuli Kasyupa,alisema hana taarifa juu ya wanachama
hao 50 kuhamia ccm,ila alisema amepata taarifa juu ya mwenyekiti kujiunga na
ccm na kusema kuwa Chadema haiteteleki kwani inawatu wengi kuliko ccm.
Akizungumza
kwa njia ya Mtandao kutoka nchini Ujerumani,mwenyekiti wa CCM wilayani
humo,Ally Mlaghila (KINANASI) alisema watu hao wanaohamia ccm wameona jinsi
serikali inavyochapa kazi hivyo wameona ni bora warudi nyumbani waungane nao
pamoja ili kusaidiana kuwatumikia wananchi.
Post a Comment