Header Ads


Wachezaji wawili wanaomzuia Aubameyang kutua Arsenal kwa sasa


Kufanikiwa kwa Arsenal kumnunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang kwa £60m kutategemea makubaliano kuhusu wachezaji wengine wawili.
Na mshambuliaji wa Gunners Olivier Giroud ndiye huenda akawa na usemi zaidi kuhusu iwapo mkataba wa kuhama kwa Aubameyang utakamilishwa kabla ya muda wa mwisho wa kuhama wachezaji kipindi hiki, Jumatano saa 23:00 GMT.
Arsenal wamekubali kulipia gharama na mikataba ya kibinafsi ya mchezaji huyo kutoka Gabon mwenye umri wa miaka 28.
Lakini Dortmund itaidhinisha hatua hiyo kama watapata mchezaji wa kuchukua nafasi yake.
Mchezaji soka wa kimataifa wa Ufaransa Giroud, mwenye umri wa miaka 31, aliorodheshwa kuwa ndiye mchezaji atakayechukua nafasi hiyo, lakini binafsi angependelea kubaki London.
Hatua ya Chelsea kuanza kumtafuta ilimpatia nafasi hiyo ya kusalia London muda unaomfaa - na hivyo basi Dortmund wameelekeza matumaini yao kwa mshambuliaji wa Chelsea Mbelgiji Michy Batshuayi, ambaye anaweza kuwa tayari kuhama.
Batshuayi akahamia Dortmund basi Chelsea wanaweza kufanikiwa kumchukua Giroud.
Batshuayi, mwenye umri wa miaka 24, amekuwa akichezeshwa sana kama mchezaji wa kuongeza nguvu mpya katika kikosi cha Chelsea na anataka kucheza zaidi kikosi cha kwanza katika mwaka wa Kombe la Dunia.
Hata hivyo, the Blues wanasita kukubali bei ya Arsenal ya kumnunua Giroud ambayo iliripotiwa kuwa ni kati ya £30m-£35m.

source:bbc swahili

No comments

Powered by Blogger.