Header Ads


MWANAMKE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BEATRICE KANGU(48)MKAZI WA MTAA WA MAKANYAGIO MANISPAA YA MPANDA MKOA WA KATAVI AMEFARIKI DUNIA GHAFLA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOA SADAKA YA SHUKRANI



MPANDA-KATAVI
Tukio  la  kifo hicho cha  mwanamke ambaye alikua mwanakwaya wa kwaya ya kigango cha makanyagio   limetokea  hapo Julai 30 majira ya saa moja  na  nusu   asubuhi  katika  Mtaa wa   Makanyagio wakati wa ibada. 

Kwamujibu wa makamu  Mwenyekiti wa  Kigango  hicho  Charles Kanyanda   ameeleza jana kuwa  siku  hiyo  Kangu  alifika  kwenye  ibada  kigangoni hapo kama   ambavyo  walivyofika  siku  hiyo  waumini  wengine kwa  ajili ya  kusali.

Kanyanda ameongeza Baada ya  mahubiri ya  Katekista   Ntalwila kuisha ilifuata   utoaji   sadaka ya shukurani  na  ndipo  mwanakwaya huyo  alipoinuka  alipokuwa   amekaa na  kwenda  kutoa sadaka ya   shukurani  na  baada ya kutowa sadaka   hiyo   alianguka   chini  ghafla.

Baada ya tukio hilo Wanakwaya  wenzake  walijaribu  kumpa  msaada hata  hivyo   hali yake  ilizidi kuwa   mbaya  na  alifariki   dunia   muda mfupi  na kuacha simanzi kubwa kwa  waumini wa kigango  hicho.

Mazishi Ya  marehemu  huyo yamefanyika  jana  katika   makaburi ya Mwanga  na   misa ya mazishi  iliongozwa na   Paroko wa  Kanisa  Katoliki   Parokia ya   Maria  Imakulata Monsinyori  Padri   George   Kisapa.

No comments

Powered by Blogger.