Header Ads


MKUU WA WILAYA YA NKASI MKOANI RUKWA, SAID MTANDA AMEAMURU KUKAMATWA MARA MOJA KWA MWENYEKITI WA SERIKALI YA KIJIJI CHA KATE



NKASI-RUKWA
Mkuu huyo wa wilaya ametoa agizo la kukamatwa kwa mwenyekiti huyo, aitwaye Joachim Sangu wakati wa mkutano uliofanyika kijijini hapo ambapo kuliibuka hoja ya kuwepo kwa mgogoro wa ardhi baina ya wafugaji na wakulima uliosababishwa na mwenyekiti huyo.

Katika mkutano huo wananchi wa kijiji hicho wakiwemo wajumbe wa Serikali ya kijiji, walilamikia kitendo cha Mwenyekiti huyo kushirikiana na afisa mtendaji wa kijiji ambaye amehamishwa hivi sasa ambao wanadaiwa kuwatoza kiasi cha Sh 500,000 kwa kila mfugaji na kuwaruhusu kuhamia kijijini hapo.

Kutokana na malalamiko hayo ya wananchi, mkuu huyo wa wilaya ameagiza kukamatwa kwa mwenyekiti huyo ambaye alikuwepo katika kikao hicho na kushindwa kujitetea kutokana na tuhuma hizo za kuruhusu mifugo hiyo kuingia pasipo kufuata utaratibu na kuchukua mamilioni ya fedha kutoka kwa wafugaji hao.

Awali, mmoja wa wakazi wa kijiji hicho, Paul James alisema kuwa wafugaji hao wapatao 50 walikaribishwa kinyemela kijiji hapo hali ambayo imeanza kusababisha kuibuka kwa migogoro ya ardhi baina ya jamii ya kifugaji na wakulima wakigombea mashamba ambayo tayari wafugaji wanadai ni sehemu ya malisho ya mifugo

No comments

Powered by Blogger.