MAHAKAMA YA MWANZO WILAYA YA MBOZI MKOANI SONGWE IMEMPANDISHA KIZIMBANI FOSTA MWAMLIMA (25) MKAZI WA KIJIJI CHA ILOLO KWA KOSA LA KUVAMIA VYOO VYA WASICHANA
MBOZI-SONGWE
Akisomewa
mashitaka hayo na Kopro Nkwimba mbele ya hakimu wa mahakama hiyo lazima
Mwaijage amesema mnamo agosti 1/ 2017 majira ya saa 11:30 alfajiri katika maeneo ya mabweni ya shule ya sekondari ya ng’amba fasto mwalima
alionekana akichungulia kwenye bafu la wasichana muda ambao wanafunzi hao
wakiwa wanaoga.
Kwa upande
wa Mkuu wa shule hiyo Christopher Mswima amekiri kutokea kwa tukio hilo shuleni
hapo na kusema kuwa tukio hilo lilianza kutokea usiku wa julai 31 ambapo watu
wasiojulikana walivaa shuleni hapo na kufungua dirisha la bweni la wanafunzi
hao na kuweza kuiba mfuko mmoja wa daftari pamoja na baadhi ya nguo za
wanafunzi.
Ameendelea
kusema kuwa majira ya alfajili waliweza kumkamata mshitakiwa huyo na kufanya
nae mahojiano ambapo amesema kuwa na
mara ya Pili kufika Shuleni hapo, lakini mshitakiwa alikana shitaka hilo na
kusema kuwa yeye hajahusika na tuhuma hizo.
Hakimu wa
Mahakama hiyo Mwaijage ameahirisha kesi hiyo hadi agosti 4 ambapo upande wa
Mshitakiwa amerudishwa tena Mahabusu baada ya kukosa Wadhamini na kuwataka
mshitakiwa na Mshitaki kuja na mashahidi pamoja na dhamana kwa upande wa mshitakiwa.
Post a Comment