WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA, AMETOA MAELEKEZO YA NAMNA YA KUMALIZA MGOGORO WA ARDHI ULIODUMU KWA ZAIDI YA MIAKA SITA, KATI YA UONGOZI WA KIWANDA CHA SARUJI MBEYA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA NANYALA, WILAYANI MBOZI MKOANI SONGWE.
MBOZI-SONGWE
Mgogoro
huo, umetokana na Kiwanda cha Saruji Mbeya, kupewa eneo la kijiji hicho
chenye ekari 2,315 na uongozi wa mkoa wa Mbeya bila ya makubaliano na
wanakijiji hali iliyosababisha wagome kuondoka.
Waziri Mkuu amewaagiza wakuu wa Mikoa ya
Songwe Luteni Mstaafu Chiku Gallawa na Mbeya amos
Makalla kukutana na kufanya mazungumzo ya kulirudisha eneo hilo mkoa wa Songwe.
Waziri
Mkuu ametoa uamuzi huo leo Jumatatu, baada
ya wananchi wa kijiji hicho kuzuia msafara wake kwa lengo la kumuelezea
changamoto yao ya kudhulumiwa ardhi yao na kukabidhiwa kwa muwekezaji bila ya
kushirikishwa.
Aidha
majaliwa Amesema Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli ni sikivu na inawajali
wanyonge ndio maana amesimama ili aweze kusikiliza kero zao na kuzipatia
ufumbuzi, hivyo amewaomba waendelee kuiamini na watarudishiwa ardhi yao.
Majaliwa ameiagiza Kampuni ya Saruji Mbeya kuondoa kesi
iliyoifungua mahakamani dhidi ya wananchi wa eneo hilo, ili waweze kukutana na
Serikali pamoja na wananchi hao kwa ajili ya kujadili namna bora ya uwekezaji
katika eneo hill.
Amesema
kiwanda hicho kilipewa eneo hilo la mkoa wa Songwe kimakosa na mkoa wa Mbeya
kwa ajili ya kupata malighafi ya kutengenezea saruji hivyo Serikali haiwazuii kulitumia eneo hilo ila
wakubaliane na wananchi kwanza.
Kwa upande
wake, Mkuu wa Mkoa wa Songwe amemshukuru Waziri Mkuu kwa kulitolea tamko suala hilo na kwamba atakutaka na Mkuu wa Mkoa
wa Mbeya kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo ili wananchi waweze kuishi kwa
amani katika ardhi yao.
Post a Comment