Header Ads


MKE WA WAZIRI MKUU, MAMA MARY MAJALIWA AMEWASIHI WANAFUNZI WA KIKE NCHINI KUJIEPUSHA NA VITENDO VINAVYOWEZA KUSABABISHA KUKATISHA MASOMO YAO.


MBOZI-SONGWE
Mary ameyasema hayo jana  alipozungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Vwawa, wilayani Mbozi mkoani songwe na kuongeza kuwa   ni vema wanafunzi hao wakatumia muda wao vizuri kwa kusoma kwa mfululizo kutoka kiwango kimoja cha taaluma kwenda kingine.

Marry  ambaye aliambatana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika ziara hiyo, amewaasa wanafunzi hao kutumia wakati huu kwa kusoma kwa bidii na kujiepusha na vitendo viovu kwani ni vizuri wakasoma hadi Chuo Kikuu na kwamba wasikimbilie kufanya mambo yasiyowahusu kwa sasa kwani mshika mawili moja lazima limponyoke.

Wakati huohuo Serikali imetunga sheria kali dhidi ya watu wanaosababisha watoto wa kike kukatisha masomo yao kwa kuwapa mimba au kuwaoa ambapo Suala la wanafunzi kupata mimba na kuendelea na masomo limekuwa mjadala katika siku za hivi karibuni baada ya Rais Magufuli kusema kwamba Serikali yake haitosomesha wanafunzi wanaopata mimba wakiwa shuleni.

No comments

Powered by Blogger.