NAIBU WAZIRI WA ELIMU MHANDISI STELLA MANYANYA AMEMUAGIZA MSIMAMIZI WA UKARABATI WA SHULE YA SEKONDARI KANTALAMBA KUHAKIKISHA KUWA WALEMAVU WANAJENGEWA VYOO VYAO NDANI YA MABWENI
Ametoa agizo hilo jana muda mfupi baada ya kufanya ukaguzi wa ukarabati wa shule hiyo iliyopo Wilayani Sumbawanga iliyopewa Shilingi Bilioni 1.1 ikiwa ni mpango wa serikali wa kuzirudishia hadhi shule kongwe nchini huku shule hiyo ikiwa imejengwa tangu 1964 na haijawahi kufanyiwa ukarabati.
“Lazima muhakikishe kwamba Mnakuwa
na vyumba maalum kwaajili ya wanafunzi wenye ulemavu na kuwawekea miundombinu
hasa kwa wale wenye ulemavu ambao mazingira yao ni magumu Zaidi, kwa
mfano mwanafunzi ana ulemavu wa miguu na anatakiwa kwenda kujisaidia hapaswi
kutambaa kwenye mikojo ya wanafunzi wenziwe hii inawapelea wao kuwa katika
mazingira hatarishi zaidi,” Alisema.
Mbali na agizo hilo pia Mhandisi
Manyanya ametoa wiki tatu ukarabati wa shule hiyo uwe umekamilika kwani
muda waliopangiwa ulikwishamalizika huku kipaumebele kikiwa ni kuhakikisha
wanafunzi wanaendelea na masomo yao katika hali ya utulivu.
“Sijaridhishwa na kasi ya ukarabati
huu hivyo tumewaongezea wiki tatu mhakikishe mnamaliza ili wanafunzi waendelee
na masomo maana yake kama mngekuwa hamwezi kumaliza kwa wakati kwanini
msingesema mapema,” Alihoji
Aidha alipokuwa anakagua bwalo la
kulia chakula wanafunzi aliagiza kutanuliwa kwa bwalo hilo baada ya kuona kuwa
bwalo hilo ni dogo na wanafunzi ni wengi kiasi ambacho ingewabidi wanafunzi hao
kula kwa zamu ili wote waweze kulitumia bwalo hilo na kuongeza kuwa ukarabati
unaofanyika ni pamoja na utanuzi wa majengo kwani ukubwa wa jengo lililopo ni
wa tangu 1964 na sasa ni 2017 hivyo haliendani na mahitaji na wakati.
Kabla ya kumaliza ziara yake shuleni
hapo aliwasisitizia wanafunzi kuwa nia ya Serikali ya awamu ya tano ni
kuhakikisha kuwa hakuna tofauti kati ya shule za serikali na shule binafsi
kuanzia huduma za majengo, elimu na vifaa vya kusomea.
Post a Comment