Header Ads


HUENDA SERIKALI HIKAFUNGA MITANDAO YA KIJAMII WAKATI WA UCHAGUZI


Mkuu wa mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya Francis Wangusi

KENYA
Huenda serikali hikafunga mitandao ya kijamii wakati wa uchaguzi. Mkuu wa mamlaka ya mawasiliano nchini Francis Wangusi anasema si lengo la serikali kuzima mitandao ila iwapo itatumiwa kuzua rabsha na uchochezi basi huenda ikalazimika kufunga mitandao. Naye mwenyekiti wa tume ya uwiano Francis Ole Kaparo anasema wasimamizi wa kurasa za whatsapp watakabiliwa kisheria iwapo kurasa hizo zitatumika kwa uchochezi. Kaparo anasema kura zaidi ya 20 za whatsapp zinafuatiliwa kwa karibu baada ya kuhusishwa na uchochezi.

No comments

Powered by Blogger.