KAMPUNI YA JUMIA YALETA HUDUMA MOMBASA
KENYA
Mtandao wa Jumia umepanua matawi yake hadi Kaunti ya Mombasa katika harakati za kuongeza mauzo yake.
Akiongea na meza yetu ya biashara murugenzi mkuu wa mtandao huo Sam Chappatte amesema mtandao wao ambao una wateja milioni 4 nchini unalenga kaunti ya Mombasa kutokana na ukubwa wake nchini.
Chappatte ameomba wakazi wa Mombasa kujaribu bidhaa zake.
Mtandao huu una miaka minne sasa nchini Kenya na una malengo ya kupanua matawi yake kote nchini.
Kampuni hii inahusika na bidhaa mbalimbali zikiwemo mashine,mavazi,simu miongoni mwa bidhaa nyingine.
Post a Comment