WILAYA NKASI MKOANI RUKWA IMEZINDUA RASMI MPANGO WA UPIGAJI CHAPA MIFUGO KATIKA KIJIJI CHA MKOLE
SONGWE-MOMBA
Akizingumza jana kwenye kikao
maalumu kilichowajumuisha watendaji kadhaa wa serikali kuanzia ngazi za kata na
wilaya afisa mifugo na uvuvi Reuben kapongo alisema zoezi hili siyo geni bali
lipo katika sheria ya mifugo iliyotungwa mwaka 2010 juu ya upigaji chapa mifugo
na kuhakikisha kuwa kila mmoja anatekeleza agizo hilo
Alisema kuwa kwa mujibu wa sheria
hiyo watakaokaidi kuipiga chapa mifugo yao watakabiliwa na adhabu kali ya
kifungo jela mwaka mmoja au kulipa faini ya Tshs,mil.2 na kuwa zoezi hili ni la
muhimu sana kulingana na faida kubwa itokanayo na mifugo kupigwa chapa hiyo.
Kapongo alidai kuwa zoezi hilo
litasaidia sana kuona kuwa mifugo inakaa katika eneo husika ikiwa ni pamoja na
kujua idadi ya mifugo katika eneo husika ukilinganisha na ukubwa wa eneo la
malisho kama linalingana na idadi ya mifugo iliyopo,sambamba na kudhibiti suala
zima la uwizi wa mifugo.
Mkurugenzi mtendaji wa wilaya Julius
Mseleche Kaondo kwa upande wake aliwataka watendaji wote watakaohusika katika
zoezi hilo kuhakikisha kuwa wanazingatia kanuni na taratibu kwa kuona kuwa kila
mmoja mifugo yake inapigwa chapa hiyo na kuwa sasa kila mmoja aende katika
vijiji vyao na kuitisha mikutano ya vijiji na kuwaelimisha wananchi juu ya
zoezi hili na umuhimu wake.
Wakuu wa idara mbalimbali za
halmashauri ya wilaya Nkasi waliwataka watendaji wanaokwenda kutekeleza agizo
hilo la kitaifa katika maeneo yao kuweka mbele uzalendo na weredi ili kuweza
kufanikisha kazi hiyo kulingana na malengo ya serikali.
Walisema kuwa zoezi ili siyo jipya
bali ni mwendelezo tu wa sheria iliyotungwa na serikali ya mifugo ya mwaka 2010
na kuwa serikali iliona kuwapo kwa faida kubwa ya kupigwa chapa mifugo na ili
tuweze kuyafikia malengo hayo ni lazima kila mmoja akatimiza wajibu wake
ipasavyo na mifugo yote ikapigwa chapa.
Post a Comment