Header Ads


UTUMIKISHWAJI NA NDOA ZA UTOTONI KWA WATOTO CHINI YA UMRI WA MIAKA 16 WASHIKA KASI KWA WAKAZI WA TARAFA YA KAMSAMBA WILAYANI MOMBA MKOANI SONGWE




 SONGWE-MOMBA

Kukithiri kwa vitendo vya ndoa za utotoni na utumikishwaji watoto chini ya umri huo,huku wengi wao wakifanyuishwa kazi za kufua mashuka katika nyumba za kulala wageni,kuchota maji na biashara mbalimbali,badala ya kwenda shule,kumeibua hisia tofauti kwa wakazi wa eneo hili.
Nivas Daud mkazi wa Kamsamba,jana,alisema watoto wengi wa umri huo wamekuwa wakivuka mto Momba na kuingia kata ya Kilyamatundu wilaya ya Sumbawanga na kufanya kazi za kufua mashuka machafu katika nyumba za kulala wageni huku wengine wakiosha vyombo na kuchota maji kwenye migahawa licha ya kujua kufanya hivyo ni kosa.
Daniel Katembo mkazi wa Kilyamatundu,alisema ukosefu wa elimu kwa baadhi ya wazazi ya kujua umuhimu wa kuwasomesha watoto hasa wa kike ndiyo chanzo cha kukithiri kwa vitendo vya utumikishwaji,na kuwa ili kuthibiti hali hiyo serikali na wadau wengine washirikiane kutoa elimu kwa wazazi hao.

Joseph Simfukwe mwenyekiti wa kijiji cha Kamsamba,amekiri kuwepo kwa hali hiyo na kusema kuwa wazazi wanaoruhusu watoto wao kufanya kazi hizo hawana elimu ya uelewa wa kumsomesho mtoto hivyo watajipanga kuhakikisha wanakomesha hali hiyo.

Diwani wa kata hiyo,Prosper Nyalali,alisema ili kudhibiti hali hiyo,ipo haja ya kuhakiki nyumba zote na kujua watoto wanao fanyishwa kazi badala ya kwenda shule na kuchukua hatua za kukomesha hali hiyo.

 
Akizungumza kwa njia ya simu,mgunge wa jimbo la Momba,David Ernest Silinde,licha ya kukiri kuwepo kwa vitendo hivyo,akaeleza hatua za kukabiriana na vitendo hivyo,ambapo alisema kwa kushirikiana na viongozi wa halmashauri wataweka mikakati ya kukomesha hali hiyo.

Hata hivyo,Juma said Ilando,mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Momba,kufuatia hali hiyo,akatoa onyo kwa wazazi na walezi wanaowatumia watoto kama mradi wa kujipatia kipato badala ya kuwapeleka shule.

Ilando alisema atawaagiza maafisa maendeleo ya jamii kutokaa maofisini na badala yake waende vijijini na kushirikiana na viongozi wa vijiji kudhibiti hali hiyo na kwa wazazi watakaoshindwa kuwapeleka watoto shule wachukuliwe hatua za kisheria.
Mkoa wa Songwe umeelezwa kukithiri kwa vitendo vya utumikishwaji kwa watoto chini ya umri huo,katika maeneo ya machimbo ya madini ya dhahabu,na maeneo mbalimbali hatua ambayo ilipelekea kushuka kielimu na kushika nafasi ya mwisho kwa ufauru kwa kidato cha 4,6 na darasa la saba na endapo hatua madhubuti hazijachukulia ufauru utakuwa ni ndoto.

No comments

Powered by Blogger.