TULIA AKSONI NAIBU SPIKA WA BUNGU LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AMEFUNGUA RASIMI MFUKO WA WANAKE WA MKOA WA SONGWE AMBAO UNASIMAMIWA NA MBUNGE WA VITI MAARUM JULIANA SHONZA.
SONGWE-MBOZI
Ufunguzi
huo umefanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mkonongo ambapo amepongeza
kwa hatua hiyo iliyofanywa na mbunge wa viti maarum Juliana shonza kwa kujitoa
kiasi cha shmilioni 20 na kuwataka
wabunge wengine wajifunze kutokana na tendo alilolifanya mbunge huyo kwa
kuwajali na kuwathamini wananchi wa mkoa wa songwe.
Aidha
aksoni amesema kuwa fedha hizo zilizotolewa ambazo zitagawa kwa vijiji vyote
mkoani hapa zifanye kazi kama ilivyokusudiwa na kuwataka akina mama kuanzisha
viwanda vidogovidogo vitakavyowakwamua kiuchumi ili kuendana na kasi ya mkoa wa
songwe kwani mkoa huu ni moja ya mikoa inayoendana na Tanzania ya viwanda.
Juliana shonza mbunge wa viti maarum mkoani songwe aesema kuwa licha ya kutimiza ahadi yake ya ya kuwasaidia kiasi hicho cha fedha pia amewataka wananchi kutoa ushilikiano ili kuweza kusaidia kupeleka mbele maendeleo ya jamii mkoa na taifa kiujumla
Post a Comment