IGP SIRRO:MARUFUKU KUANDAMANA
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro ametoa onyo akisema
wamejiweka tayari kukabiliana na watu, wakiwemo wanasiasa
wanaohamasishana kuandamana nchi nzima kinyume cha sheria.
Sirro
alisema hayo jana mjini Bariadi baada ya kukutana na wajumbe wa kamati
ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Simiyu alikokuwa ziarani kukagua utayari
wa askari wa jeshi hilo.
“Kuna
makundi ya vijana wanaojiita wana mapinduzi wanahamasishana na kupanga
kuandamana nchi nzima wakiratibiwa na chama kimoja cha siasa,
tumejipanga kuwadhibiti na tutawakamata wote bila kujali vyeo na
madaraka yao,” alisema.
Sirro
aliwataka wazazi na walezi kuwaonya na kuwazuia vijana wao kushiriki
maandamano yasiyo na kibali kwa sababu hakuna atakayevunja sheria
atakayesalimika bila kuchukuliwa hatua stahiki.
“Kuvunja
sheria ni jambo rahisi lakini madhara yake ni makubwa. Wananchi
wasijiingize kwenye mambo yakiwemo uhalifu ambayo mwishowe huwagharimu,” alisema.
Post a Comment