MAKAMU WA RAIS MHE..SAMIA SULUHU APOKEA VIFAA VYA WALEMAVU KUTOKA KUWAIT
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo
amepokea Vifaa vya Walemavu vyenye thamani ya dola za kimarekani elfu
thelathini .
Akizungumza
wakati wa kupokea vifaa hivyo Makamu wa Rais alisema kuwa anaishukuru
Serikali ya Kuwait kwa Misaada wanayotoa kwa Tanzania.
“Leo
tumepata tena msaada kutoka Kuwait wa Vifaa vya Walemavu, tumepokea
vigari vya walemavu vya aina tatu au nne tofauti, tumepokea vifaa vya
Albino,vifaa vya wasioona kuanzia vya kuangalia kwa wale wenye uwezo
mdogo mpaka vya kuandikia”
Makamu
wa Rais alisema kuwa amezungumza na Balozi wa Kuwait nchini kuhusu
mahitaji ya visima vikubwa vya maji kwenye baadhi ya maeneo yenyeshida
ya maji na ujenzi wa vituo vya upasuaji.
“Nimetoka
kwenye ziara Iringa, Simiyu na nimekuta tatizo kubwa la maji, wananchi
wanahitaji visima kwa wingi kwa hiyo nimeongea nae na ameonesha kukubali
kuchimba visima virefu kwa yale maeneo yenye ukame”.
Kwa
upande wake Balozi wa Kuwait Mhe. Jasem Al Najem alisema wanamshukuru
Makamu wa Rais kwa kutenga wakati wake siku ya leo kwa ajili ya kupokea
vifaa vitakavyosaidia ndugu zetu wenye ulemavu wa viungo na ngozi.
“Huu ni mpango kamili wa kuwasaidia walemavu wa viungo na ngozi ambao unafadhiliwa na Serikali ya Kuwait”
Aidha,
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi Ajira na Watu wenye
Ulemavu, Stella Ikupa alisema ubalozi wa Kuwait umekuwa ukifanya mambo
mengi katika nchi yetu kwa watu wenye ulemavu na leo tumepokea vifaa
vingi sana na tunawashukuru sana .
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiangalia Vifaa vya Walemavu vilivyotolewa na Serikali ya Kuwait
,pichani ni Balozi wa Kuwait nchini Jasem Al Najem (katikati) na Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi Ajira na Watu wenye
Ulemavu, Stella Ikupa . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akijaribu kusukuma kiti maalum cha magurudumu kwa ajili ya walemavu mara
baada ya kukabidhiwa na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al Najem
(kulia), wengine pichani ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Bunge, Kazi Ajira na Watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa na Msaidizi wa
Balozi wa Kuwait nchini Bi. Zainab Ally.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza wakati wa makabidhiano ya baadhi ya vifaa vya walemavu
vilivyokabidhiwa na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al Najem, wengine
pichani ni Msaidizi wa Balozi wa Kuwait Bi. Zainab Ally (kushoto) na
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi Ajira na Watu wenye
Ulemavu, Stella Ikupa . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)




Post a Comment