WAZIRI MKUU AWATAKA VIONGOZI WALIOKULA PESA ZA WAKULIMA WA KOROSHO WAZIRUDISHE
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema viongozi wa Vyama vya Ushirika waliokula
fedha za wakulima wa korosho wilayani Masasi wazirudishe na wakishindwa
mali zao zikiwemo nyumba zitauzwa ili kufidia.
Pia
Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bw. Gelasius Byakanwa
ahakikishe anawasaka viongozi wa chama Ushirika cha Msingi cha Nanyindwa
wilayani Masasi ambao wamekula fedha za wakulima na kisha kutoroka.
Amesema
viongozi wa vyama vya Ushirika katika wilaya hiyo si waaminifu, ambapo
mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya sh. bilioni 2.3 za wakulima ziliibiwa
na viongozi hao, ambapo mwaka 2017/2018 sh. bilioni 1.7 zimeibiwa.
Waziri
Mkuu alitoa maagizo hayo jana (Jumatatu, Februari 2018) alipozungumza
kwa nyakati tofauti na wananchi pamoja na watumishi wa wilaya akiwa
kwenye ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara.
Alisema
viongozi wa Ushirika wa Nanyindwa ambao wametoroka ni Michael Mkali,
Yusuph Mataula, ambapo alimuagiza Bw. Byakanwa kuwasaka na kuwafikisha
kwenye vyombo vya dola ili waweze kuchukuliwa hatua zinazostahili.
Pia
Waziri Mkuu aliwaagiza Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri
nchini kuvichunguza vyama vya Msingi katika maeneo na wakikuta kuna
kiongozi amekula fedha za wakulima wamkamate na kumchukulia hatua za
kisheria.
Alisema
wakati wa watu kuomba kuchaguliwa kuongoza vyama vya Ushirika kwa lengo
la kujitajirisha umepita na Serikali imedhamilia inawasimamia wakulima
wa mazao mbalimbali nchini wakiwemo wa korosho ili kuhakikisha nao
wananufaika.
Waziri
Mkuu alisema vyama vya Ushirika wilaya hiyo vinaongoza kwa ubadhilifu
wa fedha za wakulima ambapo wiki iliyopita Bw. Byakanwa aliwakamata
viongozi 36 wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wilayani Masasi.
Viongozi
hao ambao ni wenyeviti na makatibu wanakabiliwa na tuhuma za ubadhirifu
wa fedha za wakulima wa korosho ambazo ni zaidi ya sh bilioni 2.3,
ambazo ni malipo ya zao hilo kwa msimu wa ununuzi 2016/2017 na 2017/18.
Alisema
mbali na wafanyabiasharahao, pia Meneja wa benki ya NMB tawi la Masasi,
Aidan Msuya anaye alikamatwa kwa tuhuma za kufanya muamala wa fedha za
malipo ya wakulima sh milioni 45 kwa zaidi ya mara 11 kwa siku moja.
Waziri
Mkuu alimpongeza Bw. Byakanwa kwa hatua alizozichukua dhidi ya
viongozi hao na kumuagiza ahakikishe viongozi wote waliosababisha
ubadhirifu huo wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, FEBRUARI 27, 2018
Post a Comment