AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA BAADA YA KUPATIKANA NA HATIA YA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 7 KATAVI
Katavi
Mahakama ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemuhukumu Willson John(34)
mkazi wa Kijiji cha Simbwesa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi
kutumikia jela kifungo cha maisha baada ya
kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto (7)wakati akiwa
anaoga bafuni.
Hukumu hiyo ilitolewa
jana na hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya hiyo
Chiganga Ntengwa baada ya kuridhika
na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.
Kabla ya kusoma
hukumu hiyo hakimu Ntengwa alisema mtu
yoyote anaefanya kitendo kama alichofanya
mshitakiwa huyo anakuwa
amefanya kosa kinyume cha kifungu cha sheria
namba 130 kifungu kidogo cha kwanza na 2E cha sheria
namba 131 kidogo cha tatu cha kanuni
ya adhabu.
Alieleza kutokana na ushahidi
uliotolewa mahakamani na upande wa
mashtaka uliotolewa na mashahidi sita
akiwemo mtoto aliyebakwa ambapo mshitakiwa hakuwa na shahidi
yoyote na mahakama imeridhika na ushahidi huo
wa upande wa mashtaka.
Hakimu Ntengwa alisema
kuwa miongoni mwa ushahidi uliomtia
mshitakiwa hatiani ni ule uliotolewa na mtoto mwenyewe
aliyefanyiwa kitendo hicho pia daktari aliyemfanyia uchunguzi na
kuthibitishwa kuingiliwa kwa mtoto huyo kwenye sehemu
zake za siri na kuharibiwa hali iliyomlazimu
kumwanzishia dawa za kumkinga na maambuzi ya VVU.
Awali katika kesi hiyo mwanasheria
wa Serikali Fravian Shiyo alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa
John alitenda kosa hilo Septemba 24 mwaka huu
majira ya saa 2:30 usiku nyumbani kwao
na mtoto huyo ambako mshitakiwa
alikuwa amepanga chumba kwenye nyumba
yao wazazi wa mtoto aliyembaka na wakati antenda kosa hilo wazazi wa
mtoto huyo walikuwa wakiangalia mpira sebuleni kwenye TV.
Alieleza siku
ya tukio hilo mtoto huyo alikua
amechukua maji kwaajiri ya kuingia bafuni kuoga wakati
alipokaribia kwenye mlango wa bafuni
alimkuta mshitakiwa akiwa amesimama karibu na
mlango wa kuingilia bafuni na ndipo
mshitakiwa alipomtolea kauli na kusema wewe ingia
tuu bafuni uoge na mie nakuja kupata
haja ndogo humo humo.
Mwanasheria shiyo
alisema wakati mtoto huyo akiwa
anaendelea kuoga mshitakiwa Willson aliingia
ndani ya bafu na kumziba mdomo iliasipige kelele
mtoto huyo na kisha
na kisha alianza kumbaka na
alipomaliza alimwachia mtoto huyo
na kumwambia kuwa endapo angemwambia
mtu yeyote juu ya kitendo alichomfanyia
atamuua.
Aliendelea kuieleza mahakama
hiyo aliyebakwa
awe mwoga na asiwaambie
wazazi wake na aliingia ndani
na kumwomba Mama yake ampatie maji
ya kunawa hata hivyo mama
yake alimkatalia kumpa maji kwa kile
alichodai mbona ametoka kuoga muda si mrefu
maji ya nini tena.
Ndipo mtoto huyo
alipoingia ndani ya
chumba alichokuwa akilala hata hivyo
alishindwa kupata usingizi kutokana na maumivu yalivyozidi alimwagiza mtoto
mwezake wa kike amwite
mama yake na alipoingia chumbani
alimkuta akiwa analilia huku godoro alilokua amelalia likiwa limelowa damu na ndipo alipomtaja mtuhumiwa
kuwa ndio aliyembaka.
Kabla ya
kusomewa hukumu mshitakiwa alipewa ya nafasi
ya kujitetea kama anayosababu ya msingi
ya kuishawishi mahakama imwone hana
hatia au impunguzie adhabu.
Katika utetezi
wake mtuhumiwa alidai kuwa yeye hakutenda kosa hilo
isipokuwa ni chuki za mama
wa mtoto huyo ambaye alikuwa amemwongezea
kodi ya chumba kutoka shilingi 20,000 hadi 40,000 ambazo yeye mshitakiwa
alikataa kulipa ongezeko hilo.
Utetezi huo
ulipingwa vikali na mwendesha mashitaka
wakili wa Serikali ambae aliiomba
Mahakama itowe adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwenye jamii kwa watu wenye tabia kama hiyo
Post a Comment