AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 JELA KWA KOSA LA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 15 RUKWA
RUKWA
MAHAKAMA ya wilaya Nkasi mkoani
Rukwa imemhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30 Jela,kulwa Dase (35)
mkazi wa kijiji cha Paramawe wilayani Nkasi kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka
15.
Akisoma hukumu hiyo jana hakimu
mkazi wa mahakama hiyo Ramadhan Rugemalila alisema kuwa mahakama imeridhishwa
pasipo kuacha shaka yoyote na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na
hivyo kumuhukumu mtuhumiwa kifungo hicho.
Amesema kuwa kufuatana na mwenendo
wa kesi hiyo ambapo mashahidi wanne waliweza kutoa ushahidi upande wa
mashitaka mtuhumiwa alikutwa na hatia chini ya kifungu cha sheria f
namba 130(1) na namba (2)(e) NA 131 sura ya 16 ya kanuni ya adhabu.
Awali upande wa mashitaka ukiongozwa
na mwendesha mashitaka wa jeshi la Polisi Hamimu Gwelo uliieleza mahakama hiyo
kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Agosti 12 mwaka huu majira ya saa 8 mchana.
Aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu
kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine baada ya vitendo kama
hivyo kukithiri katika siku za hivi karibuni.
Mahakama hiyo ilipompa nafasi ya
kujitetea mtuhumiwa aliomba mahakama isimpe adhabu kali kwa maana hilo ni kosa
la kwanza kwake na anategewa na familia yake.
Baada ya utetezi huo mahakama
iliamua kutoa hukumu ya kwenda jela miaka 30.
Post a Comment