WATU WATATU MBOZI WAMEHUKUMIWA KUTUMIKIA KIFUNGO CHA MIAKA MIWILI JELA NA MIEZ SABA KILA MMOJA KWA KOSA LA KUVAMIA HIFADHI YA MSITU WA ISALALO
MBOZI - SONGWE
Mahakama
ya mwanzo vwawa mjini wilayani mbozi mkoani hapa imewahukumu watu watatu kutumikia
kifungo cha miaka miwili na miez saba jela kila mmoja au kulipa faini ya sh
million moja na laki mbili ,kwa kosa la kuvamia msitu wa hifadhi ya isalalo na kuharibu
rasilimali zilizokuwamo.
Waliohukumiwa ni FANUELI MBUZI (43) mkazi wa
nambinzo, AMANI MWANSENGA (54) mkazi wa harungu na SIAMINI TAITASI(22) mkazi wa
nambizo wilaya ya mbozi mkoani hapa.
Hakimu wa mahakama hiyo Kristina mlwilo amesema mahakama
imeridhika na ushahidi uliotolewa mahakamni hapo upande wamashitaka ikiwemo vielelezo vilivyowasilishwa
hivyo mahakama imewapa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia
ya kutenda makosa kama hayo.
Kabla ya hukumu hiyo washitakiwa walipewa nafasi ya
kujitetea ambapo wameomba wapunguziwe adhabu hiyo kwani wanafamilia
zinazowategemea hivyo kuwapa adhabu hiyo.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo namwendesha mashitaka
wa jeshi la polisi colpo nkwimba kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo tarehe
15 mwez oct mwaka huu majira ya saa mbili asbuhi na kuisababishia serikali
hasara ya shi million 8 huku wakijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Post a Comment