WAJUMBE WA CC KATA YA ICHENJEZYA WILAYANI MBOZI WAMEFANYA ZIARA FUPI YA KUTEMBELEA MIRADI MBALI MBALI YA MAENDELEO YA KATA HIYO
Mbozi
Wajumbe wa ccm kata ya ichenjezya
wilayani mbozi mkoani hapa wamefanya ziara fupi ya kutembelea maeneo mbali
mbali ya kata hiyo ikiwemo ofisi ya mtendaji lengo ikiwa ni kujua miradi ya
maendeleo mbali mbali ya kata hiyo inayoendelea.
Katika ziara
hiyo fupi iliyofanyika hivi karibuni katibu wa ccm wa kata ya ichenjezya Mussa
Charlse akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi na wajumbe wa ccm kata wametembelea eneo ujenzi wa ofisi za kata hiyo
umeanza ambapo ujenzi huo umesimama kwa muda pamoja na shule ya msingi
ichenjezya ambako ujenzi wa vyoo vya shule hiyo unaendelea baada ya vile vya
awali kuharibika vibaya.
Akihoji kuhusu
ujenzi wa ofisi hizo kusimama kwa muda katibu wa ccm kata ya inchenjezya Mussa
Charle amesema ni kwasababu gani ujenzi wa ofisi hizo umesimamishwa ilihali
ujenzi huo ulipaswa kukamilishwa mapema ili ofisi hizo ziendelee kutumika na ni
kiasi gani cha pesa ambacho kimetumika katika kufikisha ujenzi wa ofisi hizo
zilipo ambapo mpaka sasa bado ni msingi.
Akijibu
swali hilo ofisa mtendaji wa kata hiyo Marko Silwimba amesema wameamua
kusimamisha ujenzi wa ofisi hizo ili kukamilisha kwanza ujenzi wa vyoo vya
shule ya msingi ichenjezya ndipo baadae
watamalizia ujenzi wa ofisi hizo na kuhusu kiasi cha pesa kilichotumika amesema
atafatilia kujua zaidi kwani hakuwepo wakati ujenzi huo unaanza.
Kwa upande
wao Abdala Msolomi mjumbe wa ccm kata hiyo na Emil Zambi ambaye ni mwenyekiti
wa ccm kata hiyo wamehoji ni kwanini ujenzi wa vyoo vya wanafunzi wa shule hiyo
umechukua muda mrefu ili hali pesa zinachangwa lakini pia vifaa vilivyotumika
katika ujenzi huo haviendani na hali halisi ya kiasi cha pesa kilichotumika
ambacho ni zaidi ya sh million 10.
Mtendaji
huyo amesema kiasi cha pesa kilichotumika katika ujenzi wa vyoo hivyo ni halali
na kuhusu kuchelewa kukamilika kwa ujenzi huo ni wananchi kusua sua katika
utoaji wa michango na hii inatokana na wananchi wenyewe kutohudhuria mikutano
ya hadhara kujua kitu gani kinaendelea.
Post a Comment