WATU 24 WAGUNDULIKA KUUGUA UGONJWA WA KIPINDU PINDU MKOANI MBEYA HUKU WAWILI WAKIFARIKI DUNIA KUTOKANA NA UGONJWA HUO
Mbeya
WATU 24 wamegundulika kuugua ugonjwa wa kipindupindu huku
mmoja akifariki dunia wilayani Kyela mkoani Mbeya na kuzuka hofu kubwa kwa
viongozi wa serikali ngazi ya wilaya ambao wamekutana pamoja na wadau
wengine kutafuta namna ya kuutokomeza ugonjwa huo hatari.
Akitoa taarifa mbele ya kikao cha
kamati ya afya iliyokutana jana kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo,mganga mkuu
wilayani humo,Dkt,Mariam Gwere Alisema uliibuka tarehe 17/11/2017 ambapo
wagonjwa wawili walipelekwa zahanati ya Dream care iliyopo Njisi wagonjwa hao
kutoka kijiji cha mbako kata ya Ikimba.
Amesema baada ya wagonjwa hao
kuchukuliwa vipimo,walibainika kuwa wanamaambukizi ya ugonjwa huo wa
kipindupindu na siku iliyofuata walibainika wengine kutoka maeneo mbalimbali.
Ameongeza kuwa kutokana na hali hiyo
maafisa afya na wakuu wengine wa idara wametawanyika maeneo mbalimbali hasa
kata zilizo pembezoni mwa mto kiwira ambao ni chanzo kikuu cha mlipuko huo
baada ya wagonjwa wa awali kuonekana kutumia maji ya mto huo yaliwa
hayajachemshwa wala kuwekwa dawa.
Alisema mpango mkakati waliouanza ni
kuhakikisha visima vyote vinawekwa dawa za kutubu maji,na kutoa eleimu kwa umma
juu ya kuchemsha maji ya kunywa,kunawa mikono na sabuni pindi watokapo chooni
na kujenga vyoo bora na safi.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri
hiyo,Mussa Mgatta,alisema kwa sasa wametenga maeneo matatu ambayo yatatumika
kwa ajili ya kuwahifadhi na kuwatibu wagonjwa watakaobainika kuambukizwa
ugonjwa huo.


Post a Comment