SERIKALI MKOANI MBEYA YASEMA HAITAWALIPA FIDIA WALE WOTE WATAKAOPISHA MRADI WA MAJI WILAYA YA CHUNYA
CHUNYA- MBEYA
Serikali imesema haitalipa fidia kwa mwananchi yeyote
atakayezuia utekelezaji wa miradi ya maji katika Wilaya Chunya Mkoani Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema
Madusa ametoa agizo hilo alipokuwa akikabidhi kwa Mkandarasi mradi wa maji
Kitongoji cha Nyatula Kata ya Kiwanja ambapo baadhi wananchi walitaka fidia
katika maeneo yatakayopitiwa na mradi huo.
Akijibu hoja ya wananchi wa Kiwanja
Mhandisi wa Maji Wilaya ya Chunya Athanas Msangule amesema Serikali kupitia
wataalamu wake itatoa vipimo kwa eneo husika la mradi kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya Wilaya Chunya Sophia Kumbuli amesema wananchi
wanapaswa kuchukua tahadhari mapema ili kutopata hasara na kupisha vyanzo vya
maji licha ya kwamba inawezekana ikawa siyo ndani ya mita 60.
Mkuu wa Wilaya ya chunya Rehema
Madusa amesema msisitizo wa agizo la wananchi kutozuia au kukwamisha miradi ya
maji kwani ina manufaa kwa wengi na kwamba atakayebainika kuzuia au kukaidi
maagizo kutoka serikalini na kufanya hujuma ya aina yoyote ile hatua kali za
kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Mradi mpya wa maji wa Nyatula
utazilisha lita za ujazo laki tisa na sitini hivyo kuongeza kiwango cha
uzalishaji wa lita laki nne na kufikia lita milioni moja laki tatu na sitini
hivyo kuwezesha mji wa Chunya kupata maji kwa asilimia sabini na kupunguza
adha ya upatikanaji wa maji katika mji huo.
Post a Comment