WAKULIMA WILAYANI MBOZI MKOANI HAPA WAMEASWA KUZINGATIA KANUNI BORA ZA KILIMO ILI KUPATA KIPATO CHENYE TIJA
MBOZI
Wakulima
wilayani mbozi mkoani hapa wameaswa kuzingatia kanuni bora za kilimo
zinazotolewa na wataalamu wake ili kujipatia kipato chenye tija.
Wito huo umetolewa na afisa mazao wilaya ya mbozi
mkoani hapa Lydia shonyela wakati akizungumza na kituo hiki juu ya mikakati
waliyonayo katika kuhakikisha wakulima wilayani hapa wananufaika na kilimo.
Shonyela amesema katika kuhakikisha mkulima
ananufaika na kilimo wameandaa mikakati maalum ikiwa ni pamoja na kuhakikisha
pembejeo zinapatikana kwa wakati, udhibiti wa ubora wa pembejeo ikiwa ni pamoja
na dawa na mbolea na kusimamia bei elekezi iliyowekwa na serikali.
Ameongeza kwa wauzaji wa pembejeo kuhakikisha wana
vibali maalumu vya kuuza pembejeo hizo ikiwa ni pamoja na kuwa na vifaa maalumu
vya uuzaji wa pamoja na kuzingatia bei iliyowekwa na serikali kinyume na hapo
hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika kuwa tofauti na hapo.
Akizungumzia changamoto zilizopo kwa sasa katika
upande wa kilimo shonyela amesema mkulima aliyekijijini hapati fulsa kutoka katika makampuni ya usambazaji wa pembejeo
kutokuwepo soko la uhakika la mzao mabadiliko ya tabia nchi uelewa mdogo wa
wakulima kutokusafisha mazao na kutozingatia vipimo wakati wa uuzaji.
Aidha ametoa wito kwa wakulima kuhakikisha wanauza mazao
yao kwa vipimo halali kwa kutumia mizani na wakati wa kununua pembejeo
wakumbuke kudai risiti pia pembejeo hizo zinunuliwe kwa wakala anayeeleweka.
Post a Comment