WADAU MBALIMBALI WAKUTANA KUTATUA ZIRO MASHULENI
RUNGWE-MBEYA
KUFUATIA
matokeo mabaya ya ufauru kwa wanafunzi wa shule zilizopo wilayani
Rungwe mkoani Mbeya,wadau wa elimu wilayani humo,wamekutana na walimu
pamoja na viongozi wa serikali kujadili namna na kuondoa ziro mashuleni.
Wilayan
ya Rungwe ni moja ya wilaya zilizopo mkoani Mbeya ikiwa na halmashauri
Mbili ambazo ni Busokelo na Rungwe,kwa mwaka huu 2018/19 imekuwa na
matokeo yasiyoridhisha ya ufauru kwa wananfunzi,ambapo juzi wadau
wamekutana ili kujadili hali hiyo.
Wakitoa
mapendekezo kwa nyakati tofauti juu ya nini kifanyike ili kuongeza
kiwango cha ufaulu wilayani hapa wadau wa elimu walioshiriki kwenye
kongamano lilifanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe,
wamesema kuwa serikali iweke mazingira wezeshi shuleni ikiwemo kuweka
umeme.
Joshua
Kiwelo mdau wa elimu,alisema ili kuongeza ufauru,ipo haja ya kujenga
nyumba za walimu na kuboresha miundombinu ya shule, pamoja uwepo wa
mabweni kwa watoto wa kike na uwepo wa chakula cha mchana mashuleni
pamoja na kutatua changamoto ya lugha ya kufundishia.
Julieth
Mwaifwani,mdau wa elimu,alisema ukosefu wa mazingira rafiki ya
kufundishia,ikiwemo mahusiano duni kati ya walimu na wazazi chanzo cha
watoto kufanya vibaya darasani,ili kuongeza ufauru ushirikiano kiwe
kipaumbele cha kwanza.
Alisema
shule nyingi majengo yake ni chakavu,hakuna matundu ya vyoo ya
kutosha,walimu kuishi mbali na shule,walimu kutopata stahiki zao na hata
kupandishwa madaraja richa ya kuwa wamekudhi vigezo,hiyo ni changamoto
kubwa itakayozidi kudidimiza elimu wilayani humo.
Akizungumzia
changamoto hizo zilizopelekea wanafunzi kufeli,mkuu wa wilaya
hiyo,Chalya Julius,alisema baadhi ya walimu ni wazembe na watoro
kazini,hivyo amemuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo,kuchukua
hatiua,ikiwemo kupigania maslahi ya walimu.
Aidha
mkuu huyo wa wilaya,alitolea ufafanuzi sera ya elimu bure ambayo wazazi
wanapashwa kutambua umuhimu wa kusaidiana na walimu kwa ajili ya
utatuzi wa kero zilizopo na kuleta maendeleo mazuri shuleni na hasa
kuchangia vyakula ili wanafunzi wale mchana.
Hata
hivyo Chalya, alisema mzazi anaweza kuchangia uboreshaji wa huduma na
miundombinu ya shule kupitia kwa mkurugezi wa halmashauli na sio wakuu
wa shule wala mwenyekiti wa kamati na kuwa changamoto zingine serikali
itazifanyia kazi.
Nae
mkurugenzi mtendaji wa halmashauli ya wilaya ya Rungwe Leonard Peter
alisema ameyapokea maagizo ya mkuu wa wilaya na kuahidi kuwasimamia
walimu ili kuongeza uwajibikaji darasani na kutafuta mbinu mpya
itakayowezesha kuongeza ufauru mwaka 2019/2020.
Post a Comment