WANUFAIKA WA TASAF WAFURAHIA KUONDOKANA NA KUWA OMBA OMBA
BAADHI
ya wananchi wilayani Rungwe mkoani Mbeya,wameishukuru serikali kupitia
halmashauri ya wilaya hiyo,kwa kutoa misada kusaidia wakazi watokao
kwenye kaya masikini ambazo zimefanikiwa kuanzisha miradi kwa ajili ya
kujikwamua kiuchumi.
Wakazi
hao kupitia misaada hiyo ya TASAF, wameweza kuanzisha miradi ya
ujasiliamali ambayo inawaingizia kipato kinachowawezesha kusomesha
watoto wao na kuendesha maisha yao ya kila siku na kujioona wao ni sawa
na wananchi wengine.
Ernes
Anyimike,mkazi wa Tukuyu,alisema yeye ni mmoja wa wanufaika wa mpango
wa kaya masikini Tasaf,ameweza kuanzisha mradi wa ufugaji kuku wa
kienyeji ambapo amekuwa akijipatia kipato kinachowezesha kuendesha
masiaha yake na hata kusomesha watoto.
Esau
Mwamita mkazi Igogwe,alisema anaipongeza serikali kwa kuanzisha mpango
huo ambao kwa sasa wameweza kunufaika mara dufu licha ya kuwa baadhi ya
wanufaika wamekuwa wakiendesha vibaya miradi na kutopata manufaa.
Alisema
ipo haja serikali kupitia halmashauri ya wilaya hiyo kutoa elimu kwa
wanufaika kutokana na baadhi yao kutofanikiwa katika kuendesha miradi
hiyo,na kuwa tangu wapate misaada hiyo,wameweza kufanikisha mambo mengi
ikiwemo kuondokana na kuwa ombaomba.
Nsajigwa
Mkapa,mratibu wa Tasaf kata ya Kawetele alisema waliweza kuwapitia na
kuwapa ushauri wanufaika wa kata yake na kuona jinsi walivyonufaika na
sasa wameweza kusomesha watoto wao pamoja na kuwa na uhakika wa kupata
chakula mara tatu kwa siku ukilinganisha na hapo awali.
Sambamba
na hilo,amewataka wanufaika hao kutobweteka na kile wanachokipata na
badara yake waongeze juhudi ya kubuni miradi ili waongeze kipato zaidi
na kuwa kwa wale ambao wameshindwa kuongeza uzarishaji watapatiwa elimu
ili nao waweze kuongeza kipato.
Post a Comment