WAZIRI MKUU ATOA SIKU MBILI KWA MADIWANI KUMALIZA TOFAUTI ZAO
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewapa siku mbili Madiwani wa Halmashauri ya
Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya kumaliza tofauti zao zinazokwamisha
utendaji wa Halmashauri hiyo na kuendelea kufanya kazi walizotumwa na
wananchi.
Tofauti
hizo ambazo zimedumu kwa takriban mwaka mmoja zmesababisha Madiwani hao
kushindwa kufanya vikao jambo linalokwamisha shughuli za maendeleo ya
wananchi katika Halmashauri hiyo.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo (Jumamosi, Julai 29, 2017) wakati
akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela akiwa katika
ziara yake ya kikazi Mkoani Mbeya.
Amesema
ikifika Jumatatu (Julai, 31, 2017) Madiwani hao wawe wamemaliza tofauti
zao na wawaite wakuu wa Idara na kuwapa taarifa hiyo ili shughuli za
maendeleo ziendelee kutekelezwa ndani ya Halmashauri hiyo.
“Baraza
la Madiwani limegawanyika mnamgogoro tunataka uishe na mshirikiane na
mshikamane katika kufanya shughuli za maendeleo ili wananchi waweze
kupata manufaa. Mkiendeleza migongano hatutawavumilia Serikali inauwezo
wa tutalivunja baraza.”
Amesema
baadhi ya Madiwani hao wanawatetea watumishi waliosimamishwa kazi kwa
tuhuma za kuiibia Serikali mabilioni ya fedha jambo ambalo halikubaliki
na halivumiliki. “Naombeni mmalize tofauti zenu mara moja kabla
sijaondoka.”
Hata
hivyo, Waziri Mkuu ameiagiza Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa
(TAKUKURU) mkoa wa Mbeya kuhakikisha watumishi wote waliohusika katika
kula fedha za umma wanachukuliwa hatua kama alivyopendekeza Mkaguzi na
Mdhibiti wa Hesabu za Serikali(CAG).
Pia
aliwahasa watumishi wa umma kuhakikisha wanatimiza wajibu na majukumu
yao kikamilifu kwa kufanya kazi kwa bidi na kuacha ubabaishaji na
kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wawahudumie wananchi ipasavyo.
Post a Comment