MKUU WA MKOA WA RUKWA NDUGU KAMISHNA MSTAAFU ZELOTE STEPHEN AKABIDHI VIFAA KATIKA ZAHANATI YA MAZWI MANSPAA YA SUMBAWANGA
Mkuu wa mkoa wa rukwa kamishna mstaafu zelote stephen (kushoto) |
SUMBAWANGA-RUKWA Katika kuendeleza dhana ya maendeleo
hayana chama Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen
amewashirikisha madiwani wa chama cha CHADEMA katika harambee ya ghafla
iliyolenga kumalizia ujenzi wa jengo la huduma za afya ya uzazi na mtoto katika
kituo cha afya Mazwi, Manispaa ya Sumbawanga.
Harambee hiyo imefanyika muda mfupi
kabla ya Mh. Zelote Kukabidhi jumla ya vitanda vya kujifungulia 16, vitanda vya
wagonjwa 80, magodoro 80 pamoja na mashuka 200 kwa wakuu wa wilaya ikiwa ni
sehemu ya mgawo wa vifaa hivyo uliofanyika nchi nzima kupitia juhudi za Rais
Dk. John Pombe Magufuli katika kuimarisha huduma za uzazi nchini.
Akikabidhi vitanda hivyo kwa wakuu
wa wilaya za sumbawanga,nkasi na kalambo ili nao wakavigawe katika vituo vya
afya mkuu wa mkoa wa Rukwa ametumia fulsa hiyo kutoa onyo kwa baadhi ya
watendaji wa idara za Afya wenye tabia zisizo endana na maadili na kazi zao.
Mganga mkuu wa mkoa wa Rukwa DR.
Bonifasi Kasululu amemshukuru raisi kwa uamzi wa kupunguza changamoto zinazo
ikabili huduma za wajawazito nchini shukrani zinazo tolewa pia na wadau wengine
hapa sumbawanga.
Post a Comment