NAIBU WAZILI WA AFYA MAENDELEO YA JAMII JINSIA ,WAZEE NA WATOTO DR HAMISI ANDREA KIGWANGALLA AMETOA MIEZI MITATU KWA JENGO LA KITUO CHA AFYA IYULA WILAYANI MBOZI MKOANI SONGWE LIWE LIMEKAMILIKA.
Dr.hamisi kigwangalla |
SONGWE-MBOZI
Dr kigwalla
ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake leo mkoani songwe ambapo amesema kila mtumishi awajibike
kulingana na nafasi yake na sio kukaa ofisini huku wananchi wanapata taabu
ikiwa ni pamoja na kukwamisha maendeleo .
Mmoja wa
wananchi Pita mwakalinga amesema kuwa kero yao kubwa ni gari ya kubebea
wagonjwa katika kituo hicho kwani
wamekuwa wakipata tabu kwa mda mrefu kutoka kituo cha afya iyula mpaka
hospitari ya wilaya vwawa na wakati mwingine kupoteza maisha ya ndugu zao kwa
kukosa usafili wakati kituo hicho kilikuwa na gari lakini hawajui mpaka sasa gari hiyo iko wap.
Kwa upande
wake mganga mkuu wa wilaya ya mbozi janeth amesema
kuwa gari hiyo ilipata ajali mbaya maeneo ya senjele na kuuzwa kama vyuma
chakavu na kwamba hata yeye anapoingia madarakani hakulikuta gari lolote .
Post a Comment