TETESI ZA USAJILI LEO 18.7.2017
BARCA YATOA DAU UPYA KUMSAJILI VERRATTI
Barcelona wapo tayari kutoa ofa ya euro milioni 65 pamoja na Ivan Rakitic ili kumpata Marco Verratti kutoka PSG majira ya joto, kwa mujibu wa Calciomercato .
Unai Emery, kocha wa PSG ameshawahi kufanya kazi na Rakitic Sevilla na klabu hiyo inaweza kushawishika kwa sababu hiyo.
CHELSEA YAMFUKUZIA AGUERO
Chelsea inaangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, kwa mujibu wa mwandish wa AS Manu Sainz .
Bosi wa City Pep Guardiola anaaminika kuwa tayari kuruhusu dili hilo kufanyika ingawa makubaliano baina ya klabu hizo mbili hayajafikiwa.
ARSENAL YAMGEUKIA MORATA
Arsenal wamemgeukia mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata wakitaka kumsajili kuziba pengo la Alexis Sanchez, kwa mujibu wa Don Balon .
EVERTON YAMTENGEA DAU WALCOTT
Everton wanaandaa dau la paundi milioni 30 kwa ajili ya mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott, kwa mujibu wa Sunday People .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza hana uhakika wa namba kikosi cha kwanza Arsenal na Ronald Koeman anatamani kumsajili kuongeza nguvu kwenye kikosi chake.
MADRID KUMUUZA BALE
Real Madrid wapo tayari kumuuza Bale kupata fedha za kutosha kumsajili nyota wa Monaco Kylian Mbappe, kwa mujibu wa Sunday Express .
Blancos wamepania kumsajili kinda huyo majira ya joto, na Manchester United na Chelsea ni klabu zinazoitamani saini ya Bale.
LEMAR AOMBA KUTUA ARSENAL
Winga wa Monaco Thomas Lemar ameitaka klabu yake kumruhusu kujiunga na Arsenal kwa mujibu wa Daily Star .
Gunners wanajipanga kutoa ofa ya paundi milioni 45 kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, lakini mabingwa hao wa Ligue 1 wanaogopoa kupoteza wachezaji wao wengi muhimu.
STURRIDGE AKATAA KUTIMKIA CHINA
Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge amekataa kujiunga na klabu ya China Beijing Guoan, kwa mujibu wa Sunday People .
Dirisha la uhamisho la China lilifungwa Ijumaa, na meneja wa Beijing Roger Schmidt alikuwa na tumaini la kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza..
CHELSEA YATOA OFA YA €100M KWA AJILI YA HIGUIAN
Juventus wamesimamisha Chelsea katika jaribio lao kumsajili mshambuliaji wao Gonzalo Higuain, kwa mujibu wa Tuttosport .
Imeripotiwa kuwa Blues wametoa kitita cha euro milioni 100 kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina, na wanamtaka Alex Sandro pia lakini Juventus imekomaa wachezaji hao hawauzwi.
MAN UTD YAMTAKA KROOS SEHEMU YA DILI LA DE GEA
Manchester United wameitaka Real Madrid kumuingiza Toni Kroos kama sehemu ya dili la David de Gea kwa mujibu wa Daily Mirror .
Miamba hao wa Hispani wanayo nia ya kumsajili De Gea, lakini Jose Mourinho naye amesema atamruhusu kipa huyo kuondoka iwapo Mjerumani huyo atakuwa sehemu ya biashara yao.
DANILO ANATAKA KUTUA CHELSEA
Beki wa kulia Danilo anataka kujiunga na klabu ya Chelsea kufanya kazi na meneja Antonio Conte, kwa mujibu wa Daily Star .
Mbrazili huyo anatamani kujiunga na Bernabeu majira ya joto na Blues wapo tayari kumleta Ligi Kuu Uingereza.
PERISIC AKIMBIA KAMBI INTER
Ivan Perisic ameondoka kwenye kambi ya mazoezi ya Inter kufuatia tetesi za kujiunga na Manchester United, Calciomercato limeripoti.
MILAN INATAKA KUMSAJILI MODRIC
AC Milan inataka kumsajli Luka Modric, lakini inaweza kupata kipindi kigumu kumshawishi kiungo huyo wa Real Madrid kutua San Siro, kwa mujibu wa Calciomercato .
Imeripotiwa kuwa Modric amekuwa akivutiwa na Milan siku nyingi, lakini kutokana na klabu hiyo kutokuwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao, mambo hayatakuwa marahisi kwao kumpata, hata kama wataishawishi Real Madrid kumuuza.
BARCA YAANDAA DAU JIPYA KWA AJILI YA PAULINHO
Barcelona wapo tayari kuongeza dau lao kwa ajili ya Paulinho hadi euro milioni 30 wanapojipanga kwa mazungumzo zaidi na klabu ya Guangzhou Evergrande kwa ajili ya kiungo huyo, kwa mujibu wa Mundo Deportivo .
Klabu hiyo ya China tayari imeshakataa ofa ya euro milioni 20 na 25 kwa ajili ya Mbrazili huyo.
WINGA WA LIVERPOOL ATAKIWA KWA MKOPO
Winga wa Liverpool Ryan Kent anatakiwa kwa mkopo na klabu ya Uingereza Hull City inayoshiriki Championship , kwa mujibu wa Liverpool Echo .
Kent alichezwa kwa mkopo msimu uliopita akiwa na Barnsley, pia amehusishwa na tetesi za kutaka kujiunga na Birmingham City.
BONUCCI ANAMTAKA MORATA MILAN
Mchezaji mpya wa AC Milan Leonardo Bonucci ameshauri Alvaro Morata kuchagua kujiunga na miamba hao wa Serie A badala ya Chelsea, kwa mujibu wa Tuttosport .
INTER YAMFUKUZIA KEITA
Inter wanataka kuipiku Liverpool katika mbio za kumsajili kiungo wa RB Leipzig Naby Keita, kwa mujibu wa CalcioMercato .
Miamba hao wa Serie A wanaamini wanaweza kufikia makubaliano na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kabla ya kulipa euro milioni 55 zinazotakiwa kuvunja mkataba wake majira ya joto 2018.
MILAN YAMTOLEA OFA RENATO
AC Milan wametoa ofa kumsajili kwa uhamisho wa mkopo Renato Sanches kutoka Bayern Munich na kipengele kitakachowaruhusu kumnunua, kimeripoti Record .
Post a Comment