Header Ads


WANANCHI WAMEPEWA MBINU ZA KILIMO ZINAZOAMBATANA NA NA MATUMIZI YA MBEGU BORA ILI KUONGEZA THAMANI YA MAZAOKATIKA MIKOA YA MBEYA, SONGWE, RUKWA NA KATAVI



 SONGWE
Kupitia kwenye mafunzo yaliyotolewa kwenye uzinduzi wa mradi wa kundeleza zao la alizeti katika mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa na Katavi yaliyotolewa na taasisi ya mifumo ya masoko ya kilimo AMDT.

Meneja wa mradi huo Martin Mgala alisema kuwa Mradi huo umelenga kuchochea uendelezaji wa uzalishaji, usindikaji na uzalishaji wa bidhaa zilizoongezewa thamani zitokanazo na zao la alizeti umewalenga wakulima wadogo hasa wanawake  vijana na wakinababa.

Na kuongeza kuwa Kupitia mradi huo unaolenga kuwezesha upatikanaji wa mbegu bora, mfumo mzuri wa masoko ya bidhaa za alizeti, huduma za upatikanaji wa pembejeo, bima mazao na taarifa za masoko ya ukakika,  kusemakuwa kwakulimakuwa kilimo hicho ni fursa nzuri  kwa kujipatia kipato.

Mradi huu utasimamiwa na shirika la uholanzi SNV kamamtekelezaji wa shughuli za program ya AMDT katika mikoa hiyo minnme
Taasisi hiyo ya AMDT imelenga kuendeleza zao hili katika mikoa 12 nchini kote katika kipindi cha awali ndani ya miaka 3 ijayo.

Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa songwe CHIKU Galawa a amesemakuwa kunauhitaji mkubwa wa mafuta ya kupikia hivyo zao la alizeti likihudumiwa kwa njia bora  linaweza kuwakomboa wakulima wadogowadogo ilikukuza uchumi wa viwanda.

Na kuongeza kuwa serikali inatumia pesa nyingi kuagiza mafuta nje ya nchi ambapo inapelekea kukuza uchumi wan chi zinazotuletea mafuta na kusababisha shilingi  ya Tanzania kudorora.
Amepongeza mradi huo utakuwa umemkomboa mwanamke ambaye kwa kiasi kikubwa ndio muathirika wa mojakwamoja kwasbabu kwa asilimia kubwa ndiye mpishi wa jamii.

Ameshauri kuwa mradi huo uwe endelevu na ukubali kupokea mabadiliko yanayojitokeza itoefaida kwa mwananchi mmoja mmoja hasa mnyonge wachini kabisa iliiweze kuchangia uchumi wananchi.




Kwa upandewake mkuu wa mkoa wa Rukwa Zelote Stephen alishauri kuwa wakuu wote wa mikoa hiyo waungane kuunga mkono jitihada za wananchi  ili waweze kujikomboakwa kutumia kilimo cha alizeti na mikoa hiyo iwe mfano kwa nchi nzima kwa kuzarisha kisasa.

Kwa upande wake mkulima Christina kayoka alipongeza jitihada hizo na kusema kuwa majibu ya changamoto zao kuhusu zao la alizeti yamepatikana kupitia mradi huu wanaimani watajikwamua kiuchumi.
Hata hivyo mkulima kutoka songwe frenki kamanda serikali ijitahidi kurekebisha miundo mbinu iliwawezekusafirisha mazao yao kwani nichangamoto kubwa barabara hazipitiki,

Pia kamanda aligusia suala la ushuru wa mageti kuwa ni kikwazo kwa wakulima kwani pembejeo zipo juu na wanapopata kile kidogo kinachukuliwa kama ushuru.
Daudi mussa ambaye ni msindikaji  alisema kuwa katikaviwanda vyao wanakosa mbegu za alizeti kza kuzalishia mafuta kwasababu wakulima hawakai katika vikundi kukusanya ili zipatikane kwa wingi na kiwanda kizalishe kwa mwaka mzima kuliko hivi sasa kinazalisha kwa miezi mitatu tu.

Kanda hiyo iliyomaarufu kwa kuzalisha mazao mbalimbali  ikiwemo mahindi , maharage, mpunga, kahawa na tumbaku kuoneshakuwa mradi huo wa zao la alizeti linaweza kuingia katika zao litakalowainua kiuchumi kutokana na uhitaji mkubwa wa mafuta hapa nchini.
(mradi umelenga kuwafikia watu laki 5, na utafanyika mikoa12 na utakuwa endelevu)



No comments

Powered by Blogger.