JUBILEE YAAHIDI KUMALIZA UMASKINI ENDAPO WATACHAGULIWA KWA MARA YA PILI
KENYA
Serikali ya Jubilee itamaliza uskwota katika muhula wake wa pili wa uongozi. Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wanasema watahakikisha wakenya wote wanapata hati miliki za mashamba yao . Wakiongea huko pwani kwenye ziara ya kujipigia debe,wamewashtumu wapinzani wao kwa kutaka uchaguzi uhairishwe wakiwataja kama wasio na ajenda yeyote kwa taifa. Wamewaomba wenyeji kujitokeza kwa wingi Agosti nane kuwachagua viongozi wao
Post a Comment