DC SHINYANGA APIGA MARUFUKU WAGONJWA KUOMBWA FEDHA ZA KUJAZIA MAFUTA YA GARI LA WAGONJWA
Mkuu wa wilaya shinyanga Josephine Matiro |
SHINYANGA
MKUU wa Wilaya ya Shinyanga,
Josephine Matiro (pichani) amesema ni marufuku kwa wagonjwa kuombwa fedha za
kununulia mafuta ya gari ili wapate huduma ya kusafi rishwa kwenda kupata rufaa
hospitali kubwa wakati halmashauri imekwisha tenga bajeti kwa ajili ya mafuta.
Matiro aliyasema hayo mwishoni mwa
wiki wakati alipokabidhiwa gari la kubebea wagonjwa na Mbunge wa Viti Maalumu,
Lucy Mayenga katika Kituo cha Afya cha Kambarage kinachohudumia zaidi ya watu
28,500. Alisema ni marufuku mgonjwa kuombwa fedha kwa ajili ya mafuta kwenye
gari ili kupelekwa hospitali kupata rufaa kwani halmashauri imetenga fedha za
mafuta na hilo kama la uongo, alimtaka mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo
alithibitishe mbele ya wananchi.
Akizungumzia uhaba wa dawa alisema
tatizo hilo limekwisha patiwa ufumbuzi mpaka sasa anachokifahamu hakuna tatizo
hilo tena kwani serikali imekwishalifanyia kazi na malalamiko madogo madogo
yaliyokuwa yakitolewa na wananchi yamekwisha malizwa.
Naye mbunge Mayenga alisema ni
bahati kupata gari hilo kwani nchini kuna vituo vingi vya afya, hvyo ni jambo
la kushukuru kwani wasingeweza kununua gari hilo kwa haraka lenye thamani ya
zaidi ya Sh milioni 290 ikiwa bado kuna changamoto ya ukosefu wa chumba cha
upasuaji.
Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya
Wilaya ya Shinyanga, Laurent Mhembe alisema kituo hicho kilianzishwa mwaka 2010,
na kimekuwa na ongezeko la wagonjwa mwaka 2014 baada ya hospitali ya rufaa ya
mkoa kupandishwa hadhi na kuwa kituo chenye utegemezi mkubwa.
IMEANDIKWA NA
KARENY MASASY,- habarileo SHINYANGA
Post a Comment