MCHEZAJI WA ZAMANI WA YANGA ACHUKUA FOMU ZA KUGOMBEA URAISI TFF
DAR ES SALAAM
Nahodha wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Ally Mayay amechukua fomu za kuwania nafasi ya urais wa shirikisho la soka Tanzania (TFF), utakaofanyika Agosti 12.
Mayay amechukua fomu hizo saa 5
asubuhi akiwa sambamba na mchezaji wa zamani wa Simba, Mtemi Ramadhan
anayewania umakamu wa Rais.
Watia nia hao walisindikizwa na umati wa wanasoka wa zamani ambao wengi walibeba ujumbe wa kuwaunga mkono Mayay na Ramadhan.
Wachezaji
wa zamani wamejikusanya kwenye shule ya Sekondari Benjamin Mkapa na
kumsindikiza Mayay kwenda kuchukua fomu za kuwania nafasi ya urais wa
TFF.
Baadhi ya wachezaji hao ni Thomas Kipese, Madaraka
Selemani, Jamhuri Kihwelu, Mohammed Hussein 'Mmachinga ', Bakari Malima
'Jembe Ulaya ' na Salum Swedi 'Kussi'.
Post a Comment