Header Ads


KUNYWA POMBE KIASI KUMESABABISHA KIFO CHA MAMA MWENYE UMRI MIAKA 35



MOMBA-SONGWE
Na manuel kaminyoge 
Mtu mmoja Mkazi Wa iyula wilayani mbozi mkoani songwe  maria mwampashi (35) amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye mto uliopo chapwa wilayani momba  kwa sababu ya ulevi wa kupindukia

Akisimulia tukio hilo kaka wa marehemu Richard  Mwampashi amesema kuwa marehemu alitoka iyula na kufika chapwa kwaajili ya msiba wa mtoto wake na siku ya jumamosi jioni juni 17 mwaka huu aliaga na kwenda kilabuni kwaajili ya kupata pombe .

Mwampashi ameongeza kuwa ilipofika usiku hakurudi  wakajua amelala kwa mtoto wake na asubuhi wakatafuta mawasiliano na ndipo walipogundua hakurudi toka kilabuni ambapo wakiwa njiani kuelekea kilabuni walipofika kwenye mto huo waliuona mwili wa marehemu ukiwa kwenye maji na kuita msaada.

Mwenyekiti wa mtaa wa kiselia Ally Mbuba amesema kuwa tukio hilo limetokea juni 18 mwaka huu saa 8;00 asubuhi ambapo ameomba serikali iwasaidie wananchi wa eneo hilo kuwajengea daraja ili waepukane na madaraja ya miti.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa   polisi mkoani songwe Matiusi Lukasi Nyange amesema kuwa kwa uchunguzi wa Awali inaonekana  mama huyo  alikunywa pombe kupita kiasi na kusababisha kifo na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya tunduma.

Aidha kamanda nyange ametoa wito kwa wananchi mkoani songwe kutumia pombe kwa usitalabu ili uepukana na matatizo kama hayo ambayo yanaweza kuepukika .

MWISHOO
contact; 0762306521 / mwabhulye93@gmail.com

No comments

Powered by Blogger.