UNESCO WATEMBELEA MRADI WA RADIO ILEJE
ILEJE-SONGWE
Kwa muda wa
siku mbili wilaya ya Ileje mkoani Songwe ilikuwa na ugeni toka Shirika la Umoja
wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Elimu,Sayansi na Utamaduni(UNESCO).
Ziara hiyo
iliyohusisha watafiti wawili Bw.Boncani Nassor
toka Tanzania na Bi.Chashe Heallesby toka London Uingereza ililenga
redio redio ya kijamii ya Ileje Fm
inayosikia kwenye mitabendi 105.3.
Katika kikao
hicho waliweza kupata maelezo jinsi halmashauri inavyoshiki katika
kukiendesha,kukitumia kituo hicho cha redio katika kuwaletea maendeleo
wananchi.
Pamoja na
mambo mengine pia wageni hao waliweza kuupokea changamoto kadha zinazokabiri
redio hiyo ambayo kwa sasa haipo hewani kutokana na kukosa umeme kwenye minara
baada ya majenereta yaliyokuwa yakitumika kuharibika karibu miezi miwili
iliyopita.
Pia ziara
hiyo iliweza kuwakutanisha wageni hao na watangazaji,wasikilizaji na wadau
wengine wa redio ili kuweza kukamilisha safari yao ya kitafiti.
Post a Comment