SYRIA YAKUBALI KUHAMISHWA KWA WANAMGAMBO WA IS
Jeshi la Syria limeridhia, makubaliano kati ya kundi
linalojiita Dola la Kiislamu na Hezbollah yanayoruhusu kuhamishwa
wanamagmbo wa IS kutoka mpaka kati ya Syria na Lebanon kwenda mashariki
mwa Syria.
"Baada ya mafanikio ya majeshi yetu na kundi la Hizbollah
yaliyopatikana magharibi mwa Qalamoun , makubaliano yaliyofikiwa
kati ya Hezbollah na kundi la kigaidi la Daesh yameidhinishwa,"
televisheni ya Syria imesema, ikinukuu chanzo kutoka jeshini.
Bado haifahamiki iwapo makubaliano hayo yanajumuisha wanamgambo wa IS ambao wako katika upande wa Syria wa mpaka pekee ama katika ardhi pia ya Lebanon.
Makubaliano ya kusitisha mapigano yalianza kufanyakazi Jumapili asubuhi katika eneo lililokuwa linadhibitiwa na kundi la Dola la Kiislamu lililoko katika eneo la mpaka, ambako wanamgambo wamekuwa wakipigana na kundi la Hezbollah pamoja na majeshi ya Syria kwa upande mmoja na jeshi la Lebanon kwa upande mwingine.
Majeshi ya Lebanon yalitangaza kusitisha mapigano katika mpaka kati ya syria na nchi hiyo kuruhusu majadiliano kufanyika kuhusiana na wanajeshi waliokamatwa mateka na kundi la IS.
Lengo la makubaliano hayo ya kusitisha mapigano karibu na mji wa Ras Baalbek ni "kuruhusu awamu ya mwisho ya majadiliano yanayohusiana na hatima ya wanajeshi waliotekwa nyara," limesema jeshi la Lebanon katika taarifa.
Hatima ya wanajeshi waliokamatwa haijulikani
IS limekamata wanajeshi 9 mwezi Agosti 2014 baada ya kushambulia mji wa mpakani wa Arsal. Hatima ya wanajeshi hao waliokamatwa haijajulikani.Taarifa zinasema huenda wanajeshi hao wameuwawa , baada ya kupatikana miili sita ya wanajeshi hao, na bado inatafutwa miili ya wanajeshi wengine watatu.
Duru za usalama zimelieleza shirika la habari la Reuters kwamba jeshi la Lebanon limeanza majadiliano ya "upatanishi" leo Jumapili kwa ajili ya kuachiliwa wanajeshi hao.
Kaskazini mashariki mwa Lebanon kunashuhudiwa mapigano makali ya vita nchini Syria, ambapo kundi la IS na makundi mengine ya jihadi yanaongeza uwepo wao katika eneo hilo la mpaka.
Majeshi ya Lebanon na Syria yalianzisha mashambulio kila moja upande wake katika eneo hilo linalodhibitiwa na IS wiki mbili zilizopita. Majeshi ya Syria yanasaidiwa na kundi la Washia la Lebanon la Hezbollah katika mapambano hayo.
Majeshi ya Syria na Hezbollah, pia yametangaza kusitisha mapigano katika eneo hilo la magharibi mwa Syria la Qalamoun ambalo liko mpakani, televisheni ya Hezbollah ya al-Manar iliripoti leo Jumapili.
Bado haifahamiki iwapo makubaliano hayo yanajumuisha wanamgambo wa IS ambao wako katika upande wa Syria wa mpaka pekee ama katika ardhi pia ya Lebanon.
Makubaliano ya kusitisha mapigano yalianza kufanyakazi Jumapili asubuhi katika eneo lililokuwa linadhibitiwa na kundi la Dola la Kiislamu lililoko katika eneo la mpaka, ambako wanamgambo wamekuwa wakipigana na kundi la Hezbollah pamoja na majeshi ya Syria kwa upande mmoja na jeshi la Lebanon kwa upande mwingine.
Majeshi ya Lebanon yalitangaza kusitisha mapigano katika mpaka kati ya syria na nchi hiyo kuruhusu majadiliano kufanyika kuhusiana na wanajeshi waliokamatwa mateka na kundi la IS.
Lengo la makubaliano hayo ya kusitisha mapigano karibu na mji wa Ras Baalbek ni "kuruhusu awamu ya mwisho ya majadiliano yanayohusiana na hatima ya wanajeshi waliotekwa nyara," limesema jeshi la Lebanon katika taarifa.
Hatima ya wanajeshi waliokamatwa haijulikani
IS limekamata wanajeshi 9 mwezi Agosti 2014 baada ya kushambulia mji wa mpakani wa Arsal. Hatima ya wanajeshi hao waliokamatwa haijajulikani.Taarifa zinasema huenda wanajeshi hao wameuwawa , baada ya kupatikana miili sita ya wanajeshi hao, na bado inatafutwa miili ya wanajeshi wengine watatu.
Wanajeshi wa Lebanon nje kidogo ya mji wa Ras Baalbek nchini Lebanon wanaopambana na wanamgambo wa IS
Maafisa
wa usalama wa Lebanon wanasema miili inayoaminika kuwa ya
wanajeshi waliotekwa ilipatikana imezikwa karibu na mpaka na
Syria.Duru za usalama zimelieleza shirika la habari la Reuters kwamba jeshi la Lebanon limeanza majadiliano ya "upatanishi" leo Jumapili kwa ajili ya kuachiliwa wanajeshi hao.
Kaskazini mashariki mwa Lebanon kunashuhudiwa mapigano makali ya vita nchini Syria, ambapo kundi la IS na makundi mengine ya jihadi yanaongeza uwepo wao katika eneo hilo la mpaka.
Majeshi ya Lebanon na Syria yalianzisha mashambulio kila moja upande wake katika eneo hilo linalodhibitiwa na IS wiki mbili zilizopita. Majeshi ya Syria yanasaidiwa na kundi la Washia la Lebanon la Hezbollah katika mapambano hayo.
Majeshi ya Syria na Hezbollah, pia yametangaza kusitisha mapigano katika eneo hilo la magharibi mwa Syria la Qalamoun ambalo liko mpakani, televisheni ya Hezbollah ya al-Manar iliripoti leo Jumapili.
Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre
Mhariri: Caro Robi
Post a Comment