ASENSIO AISAIDIA REAL MADRID IKITOA SARE NA VALENCIA
Asensio mwenye miaka 21 alifungua ukurasa wa mabao kwa kufunga bao akiwa hatua 20 kutoka kwenye goli.Carlos Soler alisawazisha na Geoffrey Kondogbia akawaweka Valencia kifua mbele kabla ya Asensio kusawazisha kupitia mkwaju wa ikabu.
Karim Benzema - aliyepoteza nafasi nyingi nzuri - nusura awashindie Real mechi hiyo lakini mpira wake wa kichwa ulifikiwa na kipa Neto baada ya kufanya kazi ya ziada.
Real, ambao walikuwa bila mshambuliaji wao Cristiano Ronaldo aliyepigwa marufuku, walimchezesha kiungo wa kati Casemiro safu ya ulinzi kwani Sergio Ramos bado anatumikia marufuku.
Post a Comment