Header Ads


KENYA YAMALIZA YA NNE KATIKA FAINALI ZA RIADHA YA VIJANA


Kenya imemaliza ya nne kwenye mashindano ya riadha ulimwengini  kwa chipukizi wasiozidi miaka 18, mashindano yaliyofikia kikomo hapo jana jioni ugani Kasarani hapa jijini Nairobi.
Kenya ilizoa ujumla wa medali za dhahabu nne , saba za fedha na nne za shaba.  Wanariadha waliohudhuria mashindano hayo wameelezea furaha yao huku wakiwapongeza mashabiki waliofika ugani humo kwa wingi kuwaunga mkono.
Afrika kusini iliongoza jedwali la medali na ujumla wa medali kumi, Uchina walimaliza nambari mbili huku Cuba wakimaliza katika nafasi ya tatu. Ethiopia ndilo taifa lililofunga tano bora.
Medali walizopata wa wakenya.
Dhahabu
George Meitamei Manangoi – 1500 Metres
Leonard Kipkemoi Bett – 2000 Metres Steeplechase
Jackline Wambui – 800 Metres
Caren Chebet – 2000 Metres Steeplechase
Fedha
Edward Zakayo – 3000 Metres
Cleophas Kandie Meyan – 2000 Metres Steeplechase
Moitalel Mpoke Naadokila -400m Hurdles (84.0cm)
Mary Moraa – 400 Metres
Lydia Jeruto Lagat- 800 Metres
Emmaculate Chepkirui – 3000 Metres
Mercy Chepkurui -2000 Metres Steeplechase
Shaba
Japhet Kibiwott Toroitich- 800 Metres
Stanley Mburu Waithaka -3000 Metres
Dominic Samson Ndigiti – 10,000 Metres Race Walk
Edina Jebitok – 1500 Metres

No comments

Powered by Blogger.