BABY MADAHA AKILI KUFANYIWA TAMBIKO
MSANII wa
filamu na muziki Bongo, Baby Madaha Joseph, amekiri kuwa kila mwaka hurudi kwao
Mwanza kwa ajili ya kuonana na wazee wake ‘kutambika’ ambao humsaidia kufanya
mambo yake yaende vizuri mjini, kitu alichosema ni muhimu sana katika wakati
huu ambao maisha ni magumu.
Akizungumza na Za Motomoto News, Baby Madaha alisema huwa anakwenda kwao kila
mwaka na hivi sasa yupo huko kwa ajili ya kuwaona wazee wa kimila kwani huwa
wanamsaidia, hasa pale mambo yanapokuwa magumu.
“Bila wazee mambo hayaendi kabisa, niko kwetu Mwanza kwa ajili ya kufanya mambo ya kimila ili walau mambo yaende vizuri mjini maana hali imekuwa mbaya sana, nimekuwa nikifanya hivyo kila mwaka na nimeona huwa inasaidia sana,” alisema.

Post a Comment