TETESI ZA USAJILI LEO TAREHE 16.6.2017
Meneja wa Chelsea Antonio Conte amekerwa na klabu hiyo kutokubali kufanya usajili dirisha la uhamisho wa majira ya joto na anaweza kuondoka klabuni hapo kwa mujibu wa Sky Sport Italia .
Conte, ambaye aliondoka Juventus kwa sababu ya mazingira kama hayo, anataka wachezaji maalumu kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini anaona miamba hao wa London hawana mpango wa kuingia sokoni.
Bosi wa zamani wa Borussia Dortmund ametajwa kuwa mrithi wake.
REAL YAIZIDI PSG KUMFUKUZIA DONNARUMMA
Gianluigi Donnarumma Milan
Real Madrid wanaongoza katika mbio za kumsaini Gianluigi Donnarumma kutoka AC Milan, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Paris Saint-Germain, kwa mujibu wa Sky Sport Italia .
MADRID WANATAKA £78M KWA AJILI YA MORATA
Alvaro Morata Real Madrid
Real Madrid wametangaza kuwa bei ya Alvaro Morata ni paundi milioni 78 ikiwa Manchester United wanataka kweli kumsajili mshambuliaji huyo, kwa mujibu wa The Independent .
United walikuwa wakitarajia watafanikiwa kumsajili mchezaji huyo kwa kiasi cha paundi milioni 60, lakini rais wa klabu Florentino Perez amesema kwa bei hiyo mchezaji huyo hatoki.
JUVE WAKATAA OFA YA ARSENAL KWA CUADRADO
Juan Cuadrado Juventus
Dau la Arsenal la paundi milioni 17 kwa ajili ya winga wa Juventus Juan Cuadrado limekataliwa na mabingwa hao wa Serie A, kwa mujibu wa The Sun .Arsene Wenger anataka kujiandaa kwa maisha bila ya Alexis Sanchez kwenye kikosi chake na anaamini Cuadrado angeziba vema pengo la mchezaji huyo anayetaka kuondoka Emirates.Juventus wamesisitiza kuwa bila ya ofa ya paundi milioni 30 hawawezi kushawishika kumuuza mchezaji wao.
Mateo Kovacic
Arsenal na Tottenham zinapigana vikumbo kuiwania saini ya mchezaji wa Real Madrid Mateo Kovacic, kwa mujibu wa Diario Gol .Hakuna hata moja kati ya klabu hizo iliyotoa ofa kwa ajili ya mchezaji huyo raia wa Croatia, AC Milan na Inter zinatamani huduma ya mchezaji huyo pia.
ARSENAL YAMTENGEA DAU KJAER
Arsenal imetoa dau la euro milioni 12 kwa ajili ya mchezaji wa Fenerbahce Simon Kjaer, kwa mujibu wa TurksVoetbal .
Miamba hao wa Emirates watakabiliwa na ushindani kutoka kwa AC Milan ingawa klabu hiyo ya Uturuki haipo tayari kupokea fedha chini ya €15m.
FENERBAHCE YAMFUKUZIA VARDY
Fenerbahce wanajiandaa kumsajili mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy, kwa mujibu wa DHA .Miamba hao wa Uturuki wanatafuta mrithi wa Robin van Persie na pia wanataka kumsajili Ahmed Musa kutoka timu moja na Vardy.
ARSENAL YAMFUKUZIA SMALLING
Arsenal ni miongoni mwa klabu zinazofuatilia maendeleo ya beki wa Manchester United, Chris Smalling kwa mujibu wa The Sun .Mashetani Wekundu wakiwa katika harakati za kumsajili Victor Lindelof, wanaweza kumwachilia Muingereza huyo majira ya joto, West Ham nao wanataka kumsajili.
JUVE YAMFUKUZIA MAHREZ
Juventus ni klabu nyingine ya Ulaya inayotaka kumsajili winga wa Leicester City Riyad Mahrez, kwa mujibu wa Daily Mirror .Arsenal wamehusishwa na tetesi za kutaka kumsajili Mwalgeria huyo, Barcelona nayo ikiaminika kuwa moja ya timu anazoweza kujiunga nazo.
MAN UTD WANAMTAKA MATIC, SIYO FABINHO
ose Mourinho hamtaki Fabinho wa Monaco, badala yake anataka kumsajili Nemanja Matic kutoka Chelsea, kwa mujibu wa Manchester Evening News .
CHELSEA WANAMTAKA CABALLERO
Chelsea wanataka kumsajili kipa wa zamani wa Manchester City Willy Caballero kushirikiana na Thibaut Courtois, Mwandishi wa Argentina Cesar Luis Merlo amekiambia TyC Sports .
Caballero amehusishwa na tetesi za kutaka kujiunga na Newcastle baada ya kuondoka City, lakini bosi wa Chelsea Antonio Conte anamtaka kuziba pengo la Asmir Begovic, aliyejiunga na Bournemouth.
CHELSEA YAMUWINDA INSIGNE
Insigne Italy Liechteinstein
Chelsea wanajiandaa kumsajili mshambuliaji wa Napoli, Lorenzo Insigne wanapojiandaa kwa maisha bila ya Eden Hazard, kwa mujibu wa The Sun .Real Madrid wapo mbioni kutoa dau nono kwa ajili ya Hazard, na Antonio Conte anataka kupata mbadala wake haraka kuepuka usumbufu majira ya joto.
BARKLEY HURU KUONDOKA EVERTONEverton wapo tayari kumruhusu Ross Barkley kuondoka klabuni hapo majira ya joto baada ya kukataa fursa ya kuwa mchezaji anayepokea mshahara mkubwa zaidi katika klabu hiyo, kwa mujibu wa Mirror .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza amekataa dili la £100,000 kwa wiki katika Goodison Park, na sasa Ronaldo Koeman anataka kusajli wachezaji wawili kuziba pengo lake.
Post a Comment