REDIO ZATAKIWA KUWA TARISHI WA MAENDELEO
DODOMA
Wafanyakazi wa taasisi za redio wamekumbushwa wajibu wao kama ilivyo chombo chochote cha habari kuwa matarishi wa amani, upendo, mshikamano na kuhuisha maendeleo.
Wafanyakazi wa taasisi za redio wamekumbushwa wajibu wao kama ilivyo chombo chochote cha habari kuwa matarishi wa amani, upendo, mshikamano na kuhuisha maendeleo.
Aidha
wameambiwa kwamba kwa kuwa Redio ina nguvu kuliko chombo chochote
kingine duniani kwa kuwafikia watu wengi zaidi hivyo basi wanatakiwa
kuwa makini wanapowafikishia wananchi taarifa.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk.
Harrison Mwakyembe katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Waziri wa
Wizara hiyo, Juliana Shonza katika maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani
yaliyofanyika Dodoma ambaye alitaka taarifa kwa wananchi kufikishwa bila
ushabiki, chuki au kupiga chuku (kuongeza chumvi).
Alisema
tasnia ya uandishi wa Habari ni tasinia adhimu sana, hivyo Waandishi
wote wa Habari wanalo jukumu kubwa la kuzingatia misingi ya uandishi
ambayo ni mizania (balancing), kutofungamana na upande wowote
(impartiality), kutenda haki (fairness), Utu (humanity), na mwisho
kabisa kuzingatia ukweli (truthness).
Siku
ya Redio Duniani huadhimishwa kila mwaka duniani kote Tarehe 13 mwezi
Februari ili kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Redio mahali pote
duniani.
Aliwakumbusha waandishi na wageni historia ngumu na mbaya ya namna redio
zilivyotumika vibaya katika baadhi ya nchi duniani na kuleta machafuko
hadi umwagaji damu.
“Hivyo
niwaase tena kutumia redio hizo na vipaza sauti kwa ajili ya kutoa
taarifa muhimu juu ya masuala ya kilimo na ufugaji, majanga mbalimbali,
elimu juu ya sera na sheria mbalimbali za nchi, masuala ya afya kwa
jamii na elimu. Na kwa kufanya hivyo tu, ndipo tutakuwa tumeitendea haki
tasnia hii.” alisema Dk. Shonza.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana
Shonza akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Harrison
Mwakyembe katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani
zilizofanyika Mjini Dodoma.
Aidha
alipongeza kauli mbiu ya mwaka huu Redio na Michezo na kutoa rai kwa
waandishi wote wa habari kudumisha mila na desturi za Kitanzania na
kuongea Kiswahili fasaha bila kuchanganya na lugha zingine kama
Kiingereza maarufu kama Kiswanglish.
Aidha
Waziri Mwakyembe alishukuru Shirika la UNESCO na Mtandao wa Redio Jamii
Tanzania (TADIO) kwa kuwezesha siku ya redio na kusema atatafakari hoja
zote zilizowasilsihwa kwake.
Naye
Katibu wa Mtadao wa Radio Jamii (TADIO), Marco Mipawa akisoma hotuba
kwa niaba ya Mwenyekiti wa mtandao huo, Prosper Kwigize alitaka serikali
kuhakikisha kwamba urasimu unaondolewa kwenye utoaji wa taarifa kwa
umma ili kuwezesha kufanyika kwa vipindi mbalimbali vya habari.
Katibu
wa Mtandao wa Radio za Jamii nchini (TADIO), Marco Mipawa akisoma
hotuba kwa niaba ya Mwenyekiti wa Mtandao huo, Prosper Kwigize wakati
maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika mjini Dodoma kwa
ufadhili wa UNESCO.
Alitaka
Tamisemi kuweka utaratibu wa utoaji habari katika mfumo rahisi ili
wananchi wafahamu kinachotekelezwa na serikali yao. Aidha maafisa habari
walioajiriwa wapewe mamlaka na wawezeshwe kufahamu kinachofanywa na
serikali na wawe na ruhusa ya kutoa taarifa kwa vyombo vya habari katika
maeneo yao.
Aidha
alisema kutokana kutokuwa na vyanzo vya mapato ya uhakika serikali
ingeangalia suala la kodi na ushuru mbalimbali ili kusaidia Redio za
Jamii kutolipia huduma za Radio.
Pia
amesema sheria zilizopo ukilinganisha na mazingira halisi ya kazi ya
mwanahabari, mfano sheria ya Takwimu, sheria ya huduma za habari, sheria
ya makosa ya mtandao kumeshabibisha tasnia ya habari na utangazaji kuwa
katika mashaka zaidi kuliko kipindi kilichopita.
Pia
ameitaka Serikali kutoa Ruzuku ya elimu au mafunzo ya kitaaluma kwa
wanahabari ili kuwawezesha kukidhi vigezo vya kisheria ifikapo 2021
Kaimu
Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo amewataka waandishi na
watangazaji kutumia redio kwa manufaa ya taifa kuleta mshikamano na pia
kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Kaimu
Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo (wa pili kushoto)
akitoa salamu za UNESCO wakati maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani
ambapo huadhimishwa kila mwaka tarehe 13 Februari yaliyofanyika mjini
Dodoma na kuhudhuriwa na waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya
jamii kutoka Tanzania Bara na Visiwani pamoja na wadau wengine wa habari
nchini. Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith
Mahenge, Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Mh. Juliana Shonza (wa pili kulia) pamoja na Mkuu wa
Mawasiliano na Habari wa Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM), Christina
Musaroche (wa kwanza kushoto).
Aidha
alikumbusha historia ya redio na kazi iliyofanya duniani na kusema
kwamba umuhimu wa radio upo wazi na kutaka wahusika kuzitumia kwa
manufaa ya umma unaowazunguka.
Naye
Mkuu wa Mawasiliano na Habari wa Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM),
Christina Musaroche akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Kaimu Katibu
Mtendaji wa Tume hiyo Dk Moshi Kimizi, alitaka serikali na vyombo vya
habari kushirikiana katika kuhimiza michezo kwa kuwa ndicho
kinachowaleta wananchi pamoja.
Mkuu
wa Mawasiliano na Habari wa Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM), Christina
Musaroche akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Kaimu Katibu Mtendaji wa
tume hiyo Dk. Moshi Kimizi (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya
Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika Mjini Dodoma.
Alisema anadhani redio na serikali vitaona njia bora ya kutangaza michezo kwa manufaa ya taifa.
Awali
akimkaribisha Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari Mh. Shonza, Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge amesema Unesco inafanya kazi nzuri
sana kwa kuwekeza kwenye vyombo vya Habari na kuvitaka vyombo hivyo
kuitangaza Dodoma na fursa zake kwa sababu ndio makao makuu ya nchi.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge akizungumza machache
kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Mh. Juliana Shonza wakati wa sherehe za maadhimisho ya
Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika mjini Dodoma. Wa pili kulia ni
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh.
Juliana Shonza, Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith
Shayo (wa pili kushoto) pamoja na Mkuu wa Mawasiliano na Habari wa Tume
ya Taifa ya Unesco (NATCOM), Christina Musaroche (wa kwanza kushoto).
Aidha
aliitaka Redio kutangaza fursa zote ambazo zipo Dodoma ili wafanyakazi
na wafanyabiashara wanaohamia Dodoma kujua wanapata wapi mahitaji yao
yakiwemo Makazi, Maji, Chakula, Elimu na kadhalika.
Alitaka vyombo hivyo kuvutia wawekezaji ili mji huo uwe kweli katika karne ya 21 na makao makuu ya nchi.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana
Shonza akiwasili katika hoteli ya Nashera mjini Dodoma kushiriki sherehe
za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani akiwa ameambatana na Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge (kulia) pamoja na Katibu
wa Mtandao wa Radio za Jamii nchini (TADIO), Marco Mipawa (kushoto).
Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith
Mahenge, Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Mh. Juliana Shonza, Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini,
Faith Shayo pamoja na Mkuu wa Mawasiliano na Habari wa Tume ya Taifa ya
Unesco (NATCOM), Christina Musaroche wakiwa meza kuu wakati wa sherehe
za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani mjini Dodoma.
Mratibu wa Mtandao wa Vyombo vya Habari na Jinsia Kusini mwa Afrika
(GEMSAT) , Gladness Munuo akitoa mada kuhusu usawa wa jinsia katika
kuripoti michezo, changamoto na taratibu zake wakati wa sherehe za
maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika mjini Dodoma.
Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena akisisitiza
umuhimu wa maudhui katika vipindi vya redio ambapo aliwaasa kutangaza
masuala yanayowahusu wanajamii katika maeneo yanayohusika badala ya
kuwalisha wasikilizaji taarifa ambazo ziko nje na mipaka wanayoishi.
Mtaalamu wa Vyombo vya Habari na Mawasiliano, Mariagoreth Charles
akiwasilisha kanuni za uandishi wa habari za mtandaoni na mitandao ya
kijamii kwa waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya jamii kutoka
Tanzania Bara na Visiwani pamoja na wadau wengine wa habari nchini
walioshiriki kwenye maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika
mjini Dodoma.
Mtangazaji Mkongwe wa Habari za Michezo nchini, Abdallah Majura amesema
pamoja na kwamba waandishi wanatangaza vipindi vya michezo lakini
maudhui hayakidhi na kuvutia vile inavyostahili akitoa mfano hai wakati
akichangia kwa nini waandishi wengi hawaandiki habari za michezo. Majura
amesema yeye mwenyewe amewahi kupata tuzo mbili kwa ajili ya vipindi
vya michezo.
Pichani juu na chini ni sehemu ya waandishi wa habari wa vyombo vya
habari vya jamii kutoka Tanzania Bara na Visiwani pamoja na wadau
wengine wa habari nchini waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya Siku ya
Redio Duniani yaliyofanyika mjini Dodoma.
Post a Comment