WAASWA KUACHA KUENEZA PROPAGANDA MBAYA KUHUSU MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA YANAYOENDESHWA SEHEMU MBALI MBALI
MBOZI -SONGWE
Wanasiasa nchini wametakiwa kuacha kueneza
propaganda mbaya kuhusu mafunzo ya jeshi la akiba la mgambo yanayoendeshwa
sehemu mbalimbali nchini.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Mbozi John
Ernest Palingo wakati akifunga mafunzo ya jeshi la akiba la magambo katika
kijiji cha Mbozi wilayani hapa kuwa mafunzo hayo yanatambulika kisheria na yapo
kikanuni hivyo wanasiasa waache kupotosha kuwa yapo kisiasa.
Aidha palingo amewataka viongozi wa ngazi zote
kuwatumia vijana hao katika shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kupambana na
rushwa,kuokoa wananchi wakati wa majanga mbalimbali na katika shughuli za
ujenzi ili wasishawishike kufanya vitendo viovu.
Mhitimu wa mafunzo hayo Hamduni Nzowa amesema kuwa
mafunzo hayo yamewajenga na kuwa wakakamavu na kuahidi kutumia mafunzo hayo
kuisaidia jamii kwani kwa kipindi cha mafunzo hayo wamesaidia kuchimba choo
katika shule ya msingi Mbozi na kusaidia kufanya usafi katika maeneo mbalimbali.
Katibu tarafa tarafa ya igamba Kingdom Braydon
Mwambalaswa na mwenyekiti wa kijiji chaq mbozi FREDRICK SHIUGA wamesema kuwa
wataitumia nguvu kazi hiyo katika kazi za kimaendeleo na kuzuuia uhalifu katika
jamii yao ili kuimarisha ulinzi na usalama.
Kwa upande wake mshauri wa mgambo wilaya ya Mbozi
JOHN GOLIAMA amesema amesema kuwa jamii itambue kuwa hakuna upendeleo ambao
unafanyika kwa ajili ya nafasi za kujiunga na jeshi la wanachi bali kuna vigezo
vinavyotazamwa ikiwemo kigezo cha umri.
Post a Comment