MSAADA WA VITABU VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILI 12 VIMETOLEWA KATIKA SHULE ZA MSINGI 12 MKOANI SONGWE NA SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN
SHIRIKA
lisilokuwa la kiserikali Save the children la mkoani Songwe limetoa msaada wa
vitabu vya thamani ya Tsh,Milioni 12 katika shule 13 za msingi wilayani Mbozi
mkoani hapa,lengo likiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali kuinua ufauru kwa
wanafunzi.
Miungoni
mwa vitabu vilivyotolewa na shirika hilo kwa darasa la 4,5,6 na 7 ni, English, Kiswahili, Sayansi,Stadi za kazi
na Hisabati ambavyo vitagawiwa kwa kila darasa vitabu zaidi ya 100,ambavyo
vitasaidia wanafunzi kuongeza juhudi za kujisomea.
Akizungumza
siku za hivi karibuni baada ya kupokea msaada huo,kwaniaba ya walimu wenzake, Mwl,
Bertha Kamendu,alisema anaupongeza uongozi wa Shirika hilo kwa kuona umuhimu wa
elimu na kwamba vitabu hivyo vitasaidia walimu kufundisha kiurahisi kwa kuwa
kila mwanafunzi atakuwa na kitabu .
Alisema
shirika hilo linapaswa kupongezwa kwakuwa limekuwa mstari wa mbele kusaidia
watoto hasa wanafunzi wa shule zote mkoani hapa na kwamba aliuomba uongozi huo
kuendelea kusadia pale misaada mashuleni itakapohitajika kwa kuwa bado
wanakabiliwa na changamoto nyingi.
Akizungumzia
sababu ya kutoa msaada wa vitabu Meneja wa Shirika hilo,Elamu Kayange,alisema
baada ya kuona mwaka 2016/17 mkoa wa Songwe kushika mkia kwa ufauru katika
mikoa yote nchini,aliona aungane na serikali mkoani hapa kuhakikisha Songwe
inashika nafasi za juu ndiyo maana wametoa vitabu.
Alisema
suala la ukosefu wa vitabu katika shule mbalimbali mkoani hapa limekuwa
likishika kasi kwa kuliona hilo,wameanza kugawa vitabu sambamba na misaada
mingine ili wanafunzi wapate kufauru na kujiunga na kidato cha kwanza na hata
cha tano na sita ili waweze kuelekea vyuo vikuu.
Aliongeza
kuwa bado shirika hilo litaendelea kusaidi wanafunzi pindi watakapohitajika kwa
kuwa bado changamoto mashuleni zimekuwa nyingi,na kwamba kutokana na umuhimu wa
elimu watafanya hivyo na kuwataka viongozi ngazi ya vijiji,kata ,wilaya na mkoa
kuunga mkono jitihada hizo.
Akizungumza
kwaniaba ya mkuu wa mkoa wa Songwe Chiku Galawa,mkuu wa wilaya ya Mbozi John
Palingo,alisema licha ya kupongeza jitihada za shirika hilo,alisema anauhakika
elimu Mbozi na mkoa kwa ujumla itapanda kutokana na kila mwanafunzi atakuwa na
kitabu kitakachomsaidia kujisomea.
Alisema
ni aibu kwa mkoa wa Songwe kushika nafasi ya mwisho kwa ufauru katika mikoa
yote nchini,hivyo upatikanaji wa vitabu utarahisisha mwalimu kufundisha kwa
ufasaha na kusitokee tena visingizio pindi watoto watakapofeli mitihani ijayo.
Post a Comment