WAKULIMA WILAYANI MBOZI MKOANI SONGWE WAMEULALAMIKIA UONGOZI WA KIKUNDI HICHO KWA KUSHINDWA KUWALIPA FEDHA ZAO
Mbozi
Wanachama wa kikundi cha wakulima cha muungano wa hatelele
mpito coffee group wameulalamikia uongozi wa kikundi hicho kwa kushindwa
kuwalipa fedha za mauzo ya kahawa kwa kipindi cha mwaka 2016/2017.
Wakizungumza na kituo hiki wakulima
hao wamesema kuwa mpaka sasa hawajalipwa fedha zao zaidi ya milioni 30 kitendo
wanachotafsiri kama utapeli huku wakidai kuwa kikundi hicho hakina account
kinatumia ya mtu binafsi.
John Teddy amesema kuwa pale
wanapoudai uongozi wao wamekuwa wanadai kuwa hawana fedha bali fedha zao zipo
kwa watu waliokopeshwa huku kikundi hicho kikiendeshwa kwa nguvu ya kiongozi
mmoja kama kampuni lakini si kwa nguvu za wanachama wote.
Naye Rashid Msongole amesema kuwa
hakuna muhtasari ambao ulipitishwa na kikundi kizima kuruhusu ukopeshaji huo wa
fedha za kikundi huku kukiwa na mkanganyiko wa ulipaji wa fedha hizo hali
inayosababisha kushindwa kukamilisha hata ulipaji wa ada kwa watoto wao na
kuboresha mashamba yao kwa ajili ya kupata mavuno bora ya zao hilo huku wengine
wakilipwa chini ya kiwango.
Kwa Upande Wake Edward Ngwale amesema
kuwa kumekuwa hakuna uwazi wa uwepo wa account ya kikundi hicho kwa kuanisha
mwenendo mzima wa mapato ya fedha inayoingia na inayotoka huku jukumu hilo
likibaki kwa katibu pekee.
Akizungumzia kuhusu suala hilo
katibu wa kikundi hicho adam kalonge amesema kuwa waliokopa fedha ni mwenyekiti
na kamati yake na si katibu kwani yeye hajakopa na tuhuma zote zinaelekezwa
kwake kimakosa huku akikanusha kikundi hicho kutumia akaunti ya mtu
binafsi kuwa ni jambo lisilowezakana na kuwataka wafuate kanuni
walizowekeana.
Post a Comment