FUNDI UJENZI APANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA WIZI WA VIFAA VYA UJENZI
Mbozi
Mahakama
ya mwanzo vwawa mjini wilayani mbozi mkoani songwe imempandisha kizimbani
michael sichone (29) mkazi wa ilembo kwa tuhuma za wizi.
Mwendesha mashtaka wa jeshi la polisi Sabiti
Singolongo amedai mahakamani hapo mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Christina mlwilo
kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo tar 31 dec
mwaka jana maeneo ya ilolo.
Amedai mshitakiwa huyo ambaye ni fundi ujenzi aliiba fremu za milango 6, mapipa 2, mbao 5
vyote vikiwa na thamani ya shilingi milion moja na laki mbili mali ya sixtus
wilifred.
Mshitakiwa amekana shitaka hilo mbele ya hakimu wa
mahakama hiyo christina mlwilo na kwamba shitaka hilo limehahirishwa hadi tar
15 janu mwaka huu na mshitakiwa amepelekwa mahabusu baada ya kushindwa kukidhi
vigezo vya dhamana.
Post a Comment