AIBA NG'OMBE LEO NA KUKAMATWA LEO LEO MKAZI WA LUKULULU SEPHANIA ELIAS
Mbozi
Mahakama
ya mwanzo vwawa mjini wilayani mbozi mkoani songwe imempandisha kizimbani
sephania elias mkazi wa lukululu
mbembela mwenye umri wa miaka 20 kwa
tuhuma la wizi kinyume na kifungu cha sheria 265 kanuni ya adhabu sura ya 16.
Akisoma shtaka hilo mwendesha
mashtaka wa jeshi la polisi sabiti singolongo mbele ya hakimu wa mahakama hiyo
lazima mwaijega amesema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo leo asubuh maeneo ya
ichenjezya.
Mwendesha mashitaka amedai mtumiwa ameiba ng'ombe 2 wenye thaman ya sh million 1
mali ya Dickson mtega mkazi wa ichenjezya huku akijua kifanya hivo ni kosa na
ni kinyume cha sheria.
Mshitakiwa amekana kutenda kosa hilo
na hakimu wa mahakama hiyo lazima mwaijega ameahilisha kesi hiyo mpaka januri
16 mwaka huu na mshitakiwa amepelekwa mahabusu kwa kukosa mdhami.
Post a Comment