MTU MMOJA JINSIA YA KIUME MKOANI SONGWE AMEKAMTWA NA NYARA ZA SERIKALI
Jeshi
la polisi mkoani hapa linamshikilia mtu mmoja jinsia ya kiume mwenye umri wa
miaka 31 mkazi wa kijiji cha isangawana wilayani chunya mkoani mbeya kwa kosa
la kukutwa na nyara za serikali.
Kamanda wa polisi mkoani songwe mathias nyange
amesema tukio la kukamtwa kwa mtuhumiwa huyo limetokea tar 9 janu mwaka huu
majira ya 10 jioni katika msitu wa
mbagala uliopo tarafa ya kwimba wilayani songwe baada ya askari waliokuwa
katika msako maalumu kufanikiwa kumkamata.
Inadaiwa mtuhumiwa baada ya kukamatwa kwenye begi alilokua amebeba ulikutwa mkia mmoja wa
nyumbu na pua moja ya ngiri vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi mil 2
kinyume na sheria.
Kamanda ameongeza mtuhumiwa huyo hutumia nyara hizo
za serikali katika shughuli zake za uganga wa jadi ambapo hana kibali chochote
cha kuendesha shughuli hizo.
Aidha kamanda nyange amewasihi wananchi mkoani hapa
kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa jeshi la polisi, huku akiwaonya wale wanaoendelea kujihusisha
na vitendo vya uhalifu ikiwa ni pamoja na kuua wanyama pori na kutumia viungo
hivyo kipigia ramli kuacha mara moja.
Post a Comment